Nilidhani CIVIL Engineering imeshakuwa dissolved into water resources, structural & highway engineering. Well, issue ya degree VS ajira ipo complex kidogo. Kuna graduate engineers wengi sasa wameajiriwa fani tofauti kabisaaa.
Miaka mingi kidogo niliwahi kujiuliza swali kama lako na nikaomba ushauri kwa watu wengi. By then, Electrical Engineering ilikuwa hot-cake kwelikweli maana kampuni za simu ziikuwa ndo zinaanza na graduate electrical engineers walikuwa wanadakwa juu juu hata kabla hawajamaliza
Kuna mdau (electrical engineering technician) alinishauri nisisome Electrical engineering, bali nijoin Civil Engineering. Sikumbuki sababu kubwa aliyonipa ila mwisho wa siku nilijoin Civil Engineering. Sijajutia uamuzi wangu mpaka leo.