Civilian Coin: Unapokuwa Rais wa Nchi usiwe takataka, jiheshimu na ulinde usiwe na doa chafu

C-C Digital Pro

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2026
Posts
361
Reaction score
532
Unapokuwa Rais wa Nchi usiwe takataka, jiheshimu na ujilinde usiwe na doa chafu
BackgroundEraser_20260506_123831321.png
Unapopewa dhamana kubwa ya mwisho katika nchi hutakiwi kufanya Mambo ya kijinga na ya kitoto maana inaweza kushusha heshima Yako, ndio maana mtu akipewa dhamana kubwa kuna baadhi ya vitu hufutwa mitandaoni au baadhi ya tabia chafu alizokuwa nazo hufunikwa kwa nguvu ili kulinda heshima yake.

Kamara Harris makamu wa RAIS mstaafu Marekani alikuwa muigizaji lakini alipopata madaraka makubwa baadhi ya video zake ziliondolewa mitandaoni pamoja na picha chafu kwa sura ya kiongozi.

Ndio maana ili uwe RAIS inatakiwa uwe umeshafanya utukutu wako kabla au uwe umeshamaliza ujana wako Mapema ili usiwe kiongozi wa kutamani Mambo wanayofanya wananchi wako bali wananchi uwaachie wao wafanye yao.

Sasa unakuta Kiongozi wa nchi anabetua makalio mitandaoni na kucheza madisco kama bado raia wakati ni kiongozi.

Ikulu nyingi duniani huvunjika heshima kutokana na RAIS kufanya Mambo ya hovyo hovyo kama ya wananchi. Usishangae mkawa na RAIS anayeonesha anaongoza Taifa la wajinga lisilojua kumshauri RAIS afanye nini.

Kuna Mwanamziki Afrika (maarufu Kama bongo enzi za nyuma) alipopata Urais aliachana na muziki akabaki kutumikia Taifa.

Kule Liberia mchezaji maarufu wa mpira George Wear alipokuwa RAIS aliachana na maswala ya mpira na kuwaachia wananchi waoneshe uwezo wao bali yeye akawa sehemu ya kuwasapoti tu.

Leo hii kuna nchi moja Afrika RAIS wake ukiingia TikTok anakata mauno Mara anakumbatiwa kumbatiwa hovyo hovyo tu Mara anaongea Mambo ya ajabu ajabu tu Kama wananchi eti naye anataka kuwa superstar bila Kujua dhamana ya Urais ni kubwa Sana kuliko usupastaa.

RAIS wa hivyo huzaa Wananchi wa hovyo maana watamuiga anayofanya au watamdharau sana. Marais kama hawa hupinduliwa kijeshi au kwenye sanduku la kura au hulazimishwa kujiuzulu maana wanadidimiza maadili ya Taifa au kulifanya Taifa lidhalilike.

Unakuta hata watendaji wake wanajiuzulu kuogopa aibu anayo waletea kiongozi wao. Mimi CIVILIAN COIN (mtoto wa KISANDU), kwa Leo naishia hapa. Chunguzeni akili za viongozi wenu, je, wana busara au "MFALME JUHA' Leo, may 8,2026.
 
Ushaur bwana deo kisandu

Deal na siasa za kimataifa narudia tena uchambuz wako uwe wa kimataifa

Usihusishe na siasa za bongo hii n kutokana na historia yako huko nyuma wanasiasa wengi hapa bongo hawapend ukwel wala kukosolewa hasa hawa wa ELIMU MBALIMBALI KUTOKA PAKISTANI watkurudisha tena LUPANGO
 
Unapokuwa Rais wa Nchi usiwe takataka, jiheshimu na ujilinde usiwe na doa chafu
View attachment 3585543Unapopewa dhamana kubwa ya mwisho katika nchi hutakiwi kufanya Mambo ya kijinga na ya kitoto maana inaweza kushusha heshima Yako, ndio maana mtu akipewa dhamana kubwa kuna baadhi ya vitu hufutwa mitandaoni au baadhi ya tabia chafu alizokuwa nazo hufunikwa kwa nguvu ili kulinda heshima yake.

Kamara Harris makamu wa RAIS mstaafu Marekani alikuwa muigizaji lakini alipopata madaraka makubwa baadhi ya video zake ziliondolewa mitandaoni pamoja na picha chafu kwa sura ya kiongozi.

Ndio maana ili uwe RAIS inatakiwa uwe umeshafanya utukutu wako kabla au uwe umeshamaliza ujana wako Mapema ili usiwe kiongozi wa kutamani Mambo wanayofanya wananchi wako bali wananchi uwaachie wao wafanye yao.

Sasa unakuta Kiongozi wa nchi anabetua makalio mitandaoni na kucheza madisco kama bado raia wakati ni kiongozi.

Ikulu nyingi duniani huvunjika heshima kutokana na RAIS kufanya Mambo ya hovyo hovyo kama ya wananchi. Usishangae mkawa na RAIS anayeonesha anaongoza Taifa la wajinga lisilojua kumshauri RAIS afanye nini.

Kuna Mwanamziki Afrika (maarufu Kama bongo enzi za nyuma) alipopata Urais aliachana na muziki akabaki kutumikia Taifa.

Kule Liberia mchezaji maarufu wa mpira George Wear alipokuwa RAIS aliachana na maswala ya mpira na kuwaachia wananchi waoneshe uwezo wao bali yeye akawa sehemu ya kuwasapoti tu.

Leo hii kuna nchi moja Afrika RAIS wake ukiingia TikTok anakata mauno Mara anakumbatiwa kumbatiwa hovyo hovyo tu Mara anaongea Mambo ya ajabu ajabu tu Kama wananchi eti naye anataka kuwa superstar bila Kujua dhamana ya Urais ni kubwa Sana kuliko usupastaa.

RAIS wa hivyo huzaa Wananchi wa hovyo maana watamuiga anayofanya au watamdharau sana. Marais kama hawa hupinduliwa kijeshi au kwenye sanduku la kura au hulazimishwa kujiuzulu maana wanadidimiza maadili ya Taifa au kulifanya Taifa lidhalilike.

Unakuta hata watendaji wake wanajiuzulu kuogopa aibu anayo waletea kiongozi wao. Mimi CIVILIAN COIN (mtoto wa KISANDU), kwa Leo naishia hapa. Chunguzeni akili za viongozi wenu, je, wana busara au "MFALME JUHA' Leo, may 8,2026.
CHIVAYO WIDNELL NA MAMA KITAMBI BIN CHEPEO.
 
Back
Top Bottom