Clairvoyants wanapatikana Tanzania?

Clairvoyants wanapatikana Tanzania?

Chambo81

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Posts
441
Reaction score
200
Hivi hawa watu wanaoitwa Clairvoyants wanapatikana Bongo? ingawa sijui ni jinsi gani inaitwa kwa kiswaahili ila tafsiri yake ni somebody who is supposedly able to perceive things that are usually beyond the range of human sense(not astrologist) ... najua Ulaya na Asia wanapatikana ... je Tanzania wapo pia?

Kuna mtu anaweza kuniambia??
 
Mkuu Chambo81, Claovoyants bongo wapo ila wanatofauti kubwa na wale wa ulaya. Hawa claivoyants wetu wanajohusisha na ushirikina, tunguli na manyanga!. Huku ndio hii inayoitwa kupiga ramli au wale waganga wanaotumia kupandisha mizimu na kuanza kueleza mambo yaliyofichika!.

Kiukweli hawa wenye vipaji hivyo wako wengi tuu hujiita wanapandisha "mizimu" au "mashetani", tatizo ni hakuna any serious research au exploration ya nguvu za watu hawa kuzitumia kuleta maendeleo!.

Claivoyance in short ni kuzungumza na waliokufa, speaking with the dead one nayo ni some sort ya ushirikina ila wazungu wameuformalize.

Clayvoyance Kisayansi uko kwenye kundi la ESP yaani Extra Sensory Perception kwa kutumia nguvu zinazoutwa PSI yaani Parapsychology Inspiration.
 
Mi napenda zaidi hizo terms ESP na PSI.
Nitarudi.
 
Dini kutoka Ulaya na Arabuni zimewakandamiza watu hawa kwa jina la Wenye Mapepo, nk. Ni watu muhimu sana.
 
Tunakusubiri.

Nilisema ntarudi ili kujifunza zaidi.
Isipokuwa, kwa mujibu wa ESP na PSI, claovoyancy bado inasumbua vichwa vya wanasayansi.
So kusema hiyo kitu ni sawa na "ukalumanzila" wa kibongo sidhani kama ni sahihi.
 
Nilisema ntarudi ili kujifunza zaidi.
Isipokuwa, kwa mujibu wa ESP na PSI, claovoyancy bado inasumbua vichwa vya wanasayansi.
So kusema hiyo kitu ni sawa na "ukalumanzila" wa kibongo sidhani kama ni sahihi.

Si sawa kabisa na ukalumanzila wa kibongo sababu hii clairvoyancy mtu anazaliwa nayo na si ya kutafuta au kurithishwa na pia iko positive tu sio mpaka kupiga tunguli!!
 
Niliwahi kusoma katika gazeti la Jitambue nadhani ilikuwa 2003-04. Kulikuwa na habari ya Prof. mmoja wa UDSM aliyefanya utafiti kuhusu clairvoyants hapa Tanzania. Alieleza kuwa alikwenda Pemba baada ya kuambiwa kulikuwa na mtu mwenye uwezo wa kukwambia jambo linalokuja mbele yako.

Na alipofika alimkuta huyo mzee, mzee alimkaribisha wakawa na mazungumzo, kisha wakati wakiagana mzee huyo akamtakia safari njema ya kwenda USA. Prof. alishangaa aliporudi UDSM na kuambiwa ana safari ya kwenda USA. Bahati mbaya aliporudi Tanzania ili amtafute yule mzee alikuta mzee ameshatangulia mbele za haki.

Watu hao wapo hapa Tanzania, ila utasikia wanapewa majina kama vile "wachawi", "wapiga ramli", n.k. na hata humu kuna baadhi umeona wanawaita majina hayo. Nadhani ni kutokana na kutawaliwa kifikra na utamaduni wa kigeni.
 
Kweli fikra zetu zimetawaliwa sana na watu wa magharibi, ukiangalia wachina wameshika mila na tamaduni zao zimewatoa wako mbali sana, madaraja magumu wanajenga usiku, dawa zao ni za mitishamba tupu, fikra zao wamezilinda kwa nguvu zote, sasa wako mbali sana!

Hawa wakweli tunge waleo na kuwathamini nao wangefikia level fulani si haba tungekuwa hatua fulani.

Nawasilisha!
 
Vipaji vya namna hii vipo tz hata mimi nimeshwahi kukutana nao baadhi na hawana ushirikina wowote wala chale mwilini, vipawa hivi havitumiki kwakuwa tumeharibiwa akili na imani kristo na islam "Mungu pekee ndiye anayejua ya mbele" wkt hata kwenye bible tunasoma karama za namna hii zipo/zilikuwepo.

Imani ya buddha huwa wanatambulika na kupewa heshima ya kipekee
 
Niliwahi kusoma katika gazeti la Jitambue nadhani ilikuwa 2003-04. Kulikuwa na habari ya Prof. mmoja wa UDSM aliyefanya utafiti kuhusu clairvoyants hapa Tanzania. Alieleza kuwa alikwenda Pemba baada ya kuambiwa kulikuwa na mtu mwenye uwezo wa kukwambia jambo linalokuja mbele yako. Na alipofika alimkuta huyo mzee, mzee alimkaribisha wakawa na mazungumzo, kisha wakati wakiagana mzee huyo akamtakia safari njema ya kwenda USA. Prof. alishangaa aliporudi UDSM na kuambiwa ana safari ya kwenda USA. Bahati mbaya aliporudi Tanzania ili amtafute yule mzee alikuta mzee ameshatangulia mbele za haki.

Watu hao wapo hapa Tanzania, ila utasikia wanapewa majina kama vile "wachawi", "wapiga ramli", n.k. na hata humu kuna baadhi umeona wanawaita majina hayo. Nadhani ni kutokana na kutawaliwa kifikra na utamaduni wa kigeni.
Daaaah hili ndo lilikua gazeti mkombozi wa watanzania na waafrika kwa ujumla kifikra na mitazamo nalikumbuka sana hata kabla halijafungiwa na kuachiwa tena...hakika tumempoteza mtu muhimu sana katika jamii brother Munga Tehenan mwandishi mkuu wa Jitambue hakika alisupply relief kwa watu wengi.
 
Kweli fikra zetu zimetawaliwa sana na watu wa magharibi, ukiangalia wachina wameshika mila na tamaduni zao zimewatoa wako mbali sana, madaraja magumu wanajenga usiku, dawa zao ni za mitishamba tupu, fikra zao wamezilinda kwa nguvu zote, sasa wako mbali sana!! Hawa wakweli tunge waleo na kuwathamini nao wangefikia level fulani si haba tungekuwa hatua fulani.
Nawakilisha!!
Kweli mkuu....tuendelee kufunguka!!!
 
Hivi hawa watu wanaoitwa Clairvoyants wanapatikana Bongo??ingawa sijui ni jinsi gani inaitwa kwa kiswaahili ila tafsiri yake ni somebody who is supposedly able to perceive things that are usually beyond the range of human sense(not astrologist)...najua ulaya na Asia wanapatikana...je Tanzania wapo pia???kuna mtu anaweza kuniambia??

Wapo wengi tu mbona!
 
Naanza kwakukwambia 2015 uchaguzi ukifanyika mshindi atakuwa niyule anaonekana mpaka sasa kaishashinda!Ila ataporwa matokeo nahatokubali!Nchi zamagharibi zitaingilia kati,nakutakuwa naserikali mseto!
 
Back
Top Bottom