Clarence Seedorf na Kluveit wamejitakia aibu.

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Eti Seedorf ndio kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon na Kluveit ndio msaidizi wake. Seedhoff aliwahi kupewa Milan kama interm coach lakini alifukuzwa miezi michache baade. Akaenda Deportivo La coruna kama sikosei akatimuliwa. Hii inamaanisha pamoja na kuwa mchezaji mzuri huwezi kuwa kocha bora.

Bora wote wawili wangebaki huko kwao na kufundisha timu za madaraja ya chini ili kupata uzoefu. Kluvertyeye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa kocha wa timu ya taifa ya uholanzi. Hii inaonyesha bado hajiamini ndo maana anajificha kwenye vivuli vya wenzie.

Kuja kufundisha timu za taifa tena za Africa bila kuwa na uzoefu ni kuchafua cv zao. Wajiandae kupata aibu, maana soka la africa ni zaidi ya vituko.
 
Umenena vyema na tumeona matokeo..
 
Mpira umedunda.
Wamechez vizuri tu
 
kushindwa kwa timu haimaanishi moja kwa moja kuwa kocha ni mbaya. Mara nyingine wachezaji hupewa maelekezo sahihi na kufanya tofauti, mara nyingine nchi inapitia kipindi ambacho wanakosa wachezaji muhimu na mahiri ambao wanaweza kuleta mafanikio. Kuna baadhi ya makocha hupata maujiko ya bure kwa kufundisha timu ambazo zina wachezaji wenye vipaji maalumu na hata wasipofanya mazoezi yoyote wala kumsikiliza kocha wakifika uwanjani wanafanya maajabu.
 
Mmeacha kumjadili kocha wenu Amunike mnakimbilia kumjadili kocha wa Cameroon ile timu imeingia kwenye mashindano huku baadhi ya wachezaji muhimu wakijitoa kwenye mgogoro wa malipo ambalo limekuwa tatizo lao sugu
 
Seadof ni kocha mzuri sana. Ila Cameroon yenyewe ndio haina wachezaji wazuri. Hivi mule ndani nani mchezaji hodari?
 
Kocha wa Morocco vp mkuu
 
aibu gan walio pata ?? kwan mpira unamatokeo mangapi, ata wangeitoa nigeria ungekuja apa na kusema ety nwanko kanu kajitakia aibu bora angekaa nyumbn na mke wake, wabongo tunawajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…