P.S. Huyo Shivji unayesema hajui habari za walalahai aliongoza Tume ya Rais ya Masuala ya Ardhi iliyotembelea Wilaya Zote za Tanzania kasoro 2 kuzungumza na Wananchi kuhusu migogoro ya ardhi na kujionea hali halisi - amezaliwa na kukulia Kilosa huko ambako kuna Class Struggle kali ya ardhi.
Kwa kuongezea, japo si mlalahoi, ni mwananchi Nyerere type, amekuwa profesa kwa zaidi ya miaka 20, gari lake ni Toyota Starlet huku akiishi nyumba ya msajili Upanga.
Kama mwanasheria aliyebobea, angekuwa milionea, lakini ukisikia kesi yoyote inatetewa na Prof, Shivji, ujue ni kesi ngumu tena ya Msaada wa Kisheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wakati walimu wengine wa sheria wakianzia siku mahakamani kubanana na fungu, Prof. Shivji anaingia kipindi cha kwanza, saa 1:00 asubuhi. Wakati walimu wengine wakipumzika viti virefu jioni, Prof. Shivji anafundisha kipindi cha mwisho 1:00 usiku mpaka saa 2:00.
Ni miongoni mwa walimu wenye kufundisha ili mwanafunzi aelimike, kuna walimu wengine, ile ni ajira anafundisha kutimiza ajira na kupata mshahara yao.
Ukifeli somo lake unajijua umefeli kihalali wala huna haja ya apeal wakati kuna walimu wanabani huku wengine wanatoa maksi za chupi, wakinyimwa cha moto utakipata, na kuna wengine wanabania kisa kazidiwa kete mambo binafsi, au kakataliwa tuu akidhani kisa ni wewe, na usipokuwa makini, mbona disco watu tumecheza sana tuu lakini sio Shivji.
Miongoni mwa Maprof, Shivji nimemvulia kofia. Ila na wengine pia wapo!.