Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Only one true class struggle exists today and thats between "Wananchi" and "Wenye nchi".......
They may not be used, but they are still extensively analysed and form an important part of academic discourse. But it is true no western country would even dream implementing Marxist ideas; they are simply an unimplementable!
Haya ni matabaka mawili mkuu na si moja... kama lingekuwa moja sidhani kama lingepingana dhidi yake lenyewe
Huwezi kuwa na a meaningful struggle kama hamna "self awareness".
Tanzania hamna "self awareness" therefore hakuna identification, therefore hakuna a struggle to speak of.
Kuna skirmishes za hapa na pale tu, leo Mtikila anasema hivi vile, baadaye anahongwa na ana fade, kesho Mrema hivi vile, baadaye kimya.
Sisi tunazunguka around personalities na wala si policies, kwa hiyo hatuwezi kuwa na struggle ya maana.
Wtawala washa hijack tangu JUWATA, OTTU Chama cha Walimu, Jumuiya ya kinamaa, wazazi mpaka machinga wamtetekwa nyara, kijiweni kwa machinga waliochoka kabisa kuna bendera ya CCM.
Struggle itoke wapi hapo?
Mkuu unaongea kana kwamba class struggle lazima iendeshwe na hao walalahai kina Mtikila, Mrema na hivyo vyama vya ambavyo vimetekwa nyara na mabepari uchwara. Mbona huongelei mapambano kati ya wamachinga na wakuu; wafugaji/wakulima na viongozi wa wilaya; na wanaobomolewa nyumba zao na Sirikali? Au na hizi nazo unaziita 'skirmishes za hapa na pale' za hapa na pale? Alafu kumbuka class struggle haimaanishi mpaka tabaka la chini lijibu mapigo - hata likipigwa na tabaka la juu bila kujibu mapigo hiyo nayo ni class struggle!
Ninachosema ni kwamba wabongo wa tabaka la chini wame resign, hawana organization ya ku advance struggle.
Hizo unazozitaja ndiyo hizo "skirmishes" zenyewe.
Kama hamna reaction kutoka kwa tabaka la chini utaaitaje hii kama class struggle? Itakuwa more of class sufferring than class struggle.
Bongo bana, intellectual mmoja tu, point of reference ya kila mtu, Shivji, Shivji, Shivji kasema, Shivji kaandika.... wengine mpaka wanakwambia usibishane na mimi, mimi nimefundishwa na Shivji.
Sijawaji kuwaona the Shivji's of the world uswahilini, sijui wana asses vipi ulalahai, na hoi, na heri kutoka kwenye viti vya mikono kwenye ivory towers za vyuo.
Kwa kuongezea, japo si mlalahoi, ni mwananchi Nyerere type, amekuwa profesa kwa zaidi ya miaka 20, gari lake ni Toyota Starlet huku akiishi nyumba ya msajili Upanga.P.S. Huyo Shivji unayesema hajui habari za walalahai aliongoza Tume ya Rais ya Masuala ya Ardhi iliyotembelea Wilaya Zote za Tanzania kasoro 2 kuzungumza na Wananchi kuhusu migogoro ya ardhi na kujionea hali halisi - amezaliwa na kukulia Kilosa huko ambako kuna Class Struggle kali ya ardhi.
Hivi kupambana ni mpaka watu washike bunduki? Wamachinga wanapofukuzwa ili wapishe walalaheri na mashopping mall yao kisha wanapopinga na kurudi mtaani kiaina huoni hilo ni pambano la kitabaka? Wanafunzi wanapoandamana kupinga kupanda kwa nauli wakati watoto wa walalaheri na baadhi ya watoto wa walalahai wanapanda maskuli basi yenye viyoyozi huoni kuwa hiyo ni class struggle? Au unasubiri uone violent revolution ndio utaamini kuwa kulikuwa na (Silent) Class Struggle in Tanzania?
- Tuna mfano wa matabaka bado hatujawa na tabakas za kweli, isipokuwa one thing for sure tuna the ruling class, kwenye ku-create hili tumefanikiwa sana.
FMES!
Hivi kupambana ni mpaka watu washike bunduki? Wamachinga wanapofukuzwa ili wapishe walalaheri na mashopping mall yao kisha wanapopinga na kurudi mtaani kiaina huoni hilo ni pambano la kitabaka? Wanafunzi wanapoandamana kupinga kupanda kwa nauli wakati watoto wa walalaheri na baadhi ya watoto wa walalahai wanapanda maskuli basi yenye viyoyozi huoni kuwa hiyo ni class struggle? Au unasubiri uone violent revolution ndio utaamini kuwa kulikuwa na (Silent) Class Struggle in Tanzania?
...Dilunga mada hii ilianza kwa kuhoji hoja ya Shivji kuhusu 'Class Struggle in Tanzania' hivyo Shivji amekuwa kiini (Reference Point)
... Swali ni: Je, alichosema Shivji kuhusu kuwepo kwa Class Struggle hapa Tanzania ni kweli?
...Huyo Shivji unayesema hajui habari za walalahai aliongoza Tume ya Rais ya Masuala ya Ardhi iliyotembelea Wilaya Zote za Tanzania kasoro 2 kuzungumza na Wananchi...