Washambuliaji wa Simba kama wangejua kumtumia Chama basi wangefunga magoli mengi sana sana.
Boko ameshindwa kumtumia chama kabisa, kapewa pasi za wazi nyingi na amezipoteza, kule mbabane kapewa pasi yeye na goli kipa kaanguka kagongesha besela.
Kocha nadhani anamwonea aibu Boko kwakuwa ni Kepteni wa timu.
Tukitaka kushinda kimataifa nafasi ya boko ni LAZIMA ibadilishwe, acheze hata kwasi au Salamba au kama Kichuya atajirekebisha.
Ninavyo mwona uchezaji wa Boko sidhani kama ataweza kubadirika.
Anapapara sana akipewa pasi, Labda anachowaza ni kuweka rekodi ya kufunga magoli mengi tu basi.
Boko achukue mda kuangalia Clips zake za video aone anavyocheza hovyo sana.
Sitaki kumkatisha tamaa ila haonekani kujirekebisha tatizo lake.
Kule mbabane kachomekewa pasi murwaa na CCC dakika ya tisa tu. Yeye na kipa anapaparika na kumpasia kipa na kudondoka, ile ni aibu kwa mshambuliaji.
Kama ilikuwa bahati mbaya mbona huo mtindo unajirudiarudia sana ?
Hadi Leo ?
Sent using
Jamii Forums mobile app