Climate Change Is Real
Tukirudi Mwanzo kabisa katika mafundisho ya Dini, mwanadamu ndiye kiumbe pekee ambaye Mwenyezi Mungu alimpa mamlaka ya kutawala viumbe hai wote wa ardhini na majini, na kupewa mamlaka ya kuitunza Dunia pamoja na viishivyo Duniani. Let's look at Genesis 1:28
“Mungu akawabariki, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi." Nimegusia maandiko haya ya kiimani kidogo hili kila mmoja wetu aweze kujua kwamba tokea mwanzo wa uumbaji katika Dunia hii na mpaka sasa tulipo Mwanadamu ndiye kiumbe pekee ambaye Mwenyezi alimpa mamlaka ya kuitawala Dunia na Kuitunza, kila unachokiona katika Dunia hii kipo kwa sababu, Kwanzia miti, ndege, wadudu, nyoka na viumbe hai wengine wote ni jukumu letu kivitunza kwa kizazi cha sasa na baadae. Please Don't Forget Our Nature Mission.
EVOLUTION OF MAN
Lakini ukikaa na kufatilia vizuri stage za maisha ya Mwanadamu alizopitia kwanzia Early, Middle and Late Stone Age hakika utagundua Mwanadamu ni kiumbe wa pekee mwenye akili nyingi sana ambaye aliweza kuzitatua changamoto za maisha katika kila stage aliyopitia. Let's start with
Early Stone Age - Hakuna kipindi ambacho Mwanadamu aliishi kwa amani na ustaarabu na mazingira kama kipindi hiki, lakini kabla sijaendelea mbele naomba wote tujue neno Stone Age linamaanisha nini? Ni kipindi ambacho Mwanadamu alitegemea sana Mawe kama Nyenzo kuu ya kifaa chake cha kazi pamoja na silaha yake ya kujikinga na kuwindia ilikuweza kupata chakula chake cha kila siku. Katika kipindi hiki Mwanadamu alitegemea mawe kwa asilimia kubwa katika shughuli zake za kila siku. Lakini pia mwanadamu aliishi maisha ya
Nomadic Lifestyle - (Ni mtu wa kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine). Kwa sababu hiyo alikuwa hana Permanent Settlement na kuweza kuyapa nafasi Mazingira uwezo mkubwa wa
Kujigenereta (kujitengeneza upya) ukizangatia population numbers ya mwanadamu kwa zama hizi almost ilikuwa is equal to zero. Lakini ni kipindi ambacho Mwanadamu alikuwa bado haja discover Fire kwa hiyo aliishi kwa kula sana matunda ya miti, mizizi na kuwinda kwa kiasi. Kwa nini nimeongelea hili la Moto, hakuna kitu muhimu kwenye maisha yetu lakini pia kina uharibifu mkubwa kwenye mazingira kama moto, japo ni one of the strong source of energy. Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa movie, kuna Movie inaitwa
Jungle Book iliyotoka mwaka 2016 na Director wa hii Movie anaitwa
Jonathan Favreau chini ya Production Company ya
Walt Disney Pictures. Main issue katika hii movie ni Red Flower (Moto), ukiutumia ndivyo sivyo basi utateketeza kila kitu na kugeuza Mbuga, Msitu au Hifadhi kuwa Jangwa na kuleta madhara makubwa kwenye mazingira na kuweza kusababisha mabadiliko ya tabia nchi. Mbali na moto katika zama hizi Mwanadamu aliishi kwa kiasi, aliwinda kwa kiasi, alikula matunda kiasi kulingana na mahitaji husika ya siku hiyo alikuwa hana muda wa kuwaza kesho akiamka atakula nini, kwa hiyo hii iliweza kusaidia kufanya rate ya uharibifu wa mazingira katika kipindi cha Early Stone Age kuwa mdogo sana ulinganisha na zama nyingine. Hebu turudi kwenye kizazi chetu cha leo unakuta binadamu wa leo, nyama anaweka kwenye Freezer hata kilo 50 mpaka 100 ya kula leo na hata mieze mitatu mbele inayokuja😋, sema tunda lolote unalotaka nyumbani kwake utalikuta ndani ya Friji yake mpaka mengine yanaozea humo humo. Kwa hiyo ukimwangalia vizuri mwanadamu ameundergo transformation za different lifestyle ambazo zimemfanya hawe mbinafsi na kujiangalia yeye kama ndiye center of Universe na kusahau viumbe hai wengine pamoja na mazingira yanayomzunguka. I hope kesho tutaendelea na segment nyingine tena kulingana na maswali yaliyoulizwa, Ahsante Sana.