Climate finance; kitanzi cha nchi masikini katika sura ya ufadhili

Joined
Feb 13, 2017
Posts
9
Reaction score
16
climate finance.jpg

AHADI za fedha kutoka mataifa tajiri kwenda mataifa masikini kwa ajili ya kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ni tamu, lakini kiuhalisia ni mtego wa madeni.

Uchambuzi wa kina unabainisha kuwa fedha hizo zinaelekezwa kusikostahili, ambapo nyingi huenda kuchangia mabadiliko ya tabianchi kuliko kutafuta ufumbuzi wake.

Mataifa masikini, Tanzania kiwemo, hulazimika kugharamia athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi mara kwa mara, ni gharama zinazojirudia, kujenga upya majengo yaliyoharibika na upotevu mapato. Katika kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi, mataifa haya masikini hutumia trilioni za fedha, na kila majanga yanapotokea hulazimika kukopa ili kujinusuru.

Matokeo ya utafiti wa ActionAid, mwaka uliopita, yanaonyesha kuwa asilimia 93 ya nchi zilizo kwenye mazingira hatarishi zaidi kwa mabadiliko ya tabianchi zinakabiliwa na hali mbaya ya madeni au kuwa katika hatari ya kutumbukia kwenye hali mbaya ya madeni, hivyo kushindwa kuwekeza kwenye elimu, afya, maji na shughuli za mabadiliko ya tabianchi.

Mfumo wa utoaji wake upo kimkakati zaidi, ukitekelezwa kama ufadhili wa fedha za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini wakati huo huo sehemu kubwa ya fedha hizo zikitolewa kwa utaratibu wa mikopo badala ya misaada, na hali hii inathibitishwa na uchambuzi wa karibuni wa Shirika la Kimataifa la Oxfarm unaoelezea kuwa theluthi mbili ya fedha hiyo ilitolewa katika utaratibu wa mikopo.

Baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya haki katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (climate justice) wanaonyesha hofu yao kuhusu mfumo wa utoaji fedha hizo wakisema hauzisaidii nchi masikini na badala yake huzinufaisha zaidi nchi tajiri ambao ndio wahusika wakuu katika uzalishaji hewa chafu duniani.

Watetezi wa uwepo wa haki katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wanashinikiza mataifa tajiri (Global North) kusaidia mataifa masikini (Global South) katika juhudi zao za kuhimili na kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa ndio waathirika wa uchafuzi wao wa hali ya hewa duniani.

“Kinachofanyika kwenye utaratibu wa sasa wa fedha za ufadhili wa athari za mabadiliko ya tabianchi ni kuziweka nchi masikini kwenye mtego wa madeni,” anasema Teresa Anderson, kiongozi wa masuala ya haki katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kutoka Shirika la Kimataifa ActionAid.

Katika mjadala kwa njia ya mtandao ulioandaliwa kwa pamoja kati ya ActionAid na Taasisi ya Mazingira, Sayansi, Afya na Kilimo (MESHA), Bi Teresa alibainisha jambo moja, kwamba mataifa tajiri hayako tayari kutekeleza wajibu wao huo kwa mataifa masikini, na kueleza kuwa upo upinzani mkali kwenye utekelezaji wa wajibu huo pamoja na utoaji fedha.

Mathalani, ni takribani miaka kumi sasa tangu mataifa tajiri duniani yakubaliane pale jijini Paris Ufaransa, mwaka 2015, kwa pamoja kutoa dola za kimarekani bilioni 100 kwa nchi masikini kila mwaka kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.

Wadau wa mabadiliko ya tabianchi duniani, wakiwemo shirika hilo la ActionAid wanaamini kuwa, sio tu kwamba kiwango hicho ni kidogo sana, bali pia sehemu kubwa ya hiyo pesa ni mikopo na sio misaada hivyo kuzibebesha nchi masikini mzigo wa madeni usiobebeka, na matokeo yake ni kushindwa kukuza uchumi wao na kutoa huduma bora za kijamii zikiwemo, afya, elimu na maji.

Pamoja na kiwango kuwa kidogo, bado mataifa hayo tajiri hayajalifikia lengo la kiwango cha utoaji ahadi hiyo kikamilifu.

Katikati ya hadaa hii, ni muhimu pia kufahamika kwamba biashara ya hewa ukaa (carbon credit), sio sehemu ya fedha kwa ajili ya kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kama inavyotangazwa na watetezi wake, na hapa Teresa anasema,

“Hainufaishi nchi masikini, bali inawanufaisha wachafuzi wa hewa pekee kwa kuwapa fursa ya kudai kwamba wanathamini mazingira safi.”

Hali halisi inaonyesha kutoshughulikiwa kwa tatizo la msingi, sababu ikitajwa kuwa wahusika wakuu wa uchafuzi wakiwemo binadamu, nchi na makampuni, hawaguswi kwa kiwango kikubwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ni watu na jamii masikini wasiohusika na uchafuzi wa hali ya hewa, ndio wenye kuathirika zaidi na athari za uchafuzi huo, ikiwemo mafuriko, ukame na kuongezeka kwa kina cha maji baharini.

Orodha ya athari za mabadiliko ya tabianchi zinazowakabili wananchi na jamii kwenye nchi masikini ni ndefu, lakini kwa uchache ni pamoja na wakulima kukabiliwa na tatizo la mazao yao kuharibika, njaa, majanga yenye kusababisha kubomoka kwa makazi yao na watoto wa kike kunyimwa fursa za elimu kutokana na kuyumba kwa kipato cha familia.

Wanawake na watoto katika nchi hizi masikini ndio waathirika wakuu wakati wa majanga wakikabiliwa na vifo, wanawake hupunguza milo yao kuziokoa familia zao, huelemewa na mzigo wa malezi ya familia, kuhangaika na watoto kipindi cha mafuriko, na kukosa huduma ya maafisa ugani

Upo ulazima sasa wa kufikiwa kwa lengo jipya la fedha za kugharamia athari za mabadiliko ya tabianchi, kuanzia mwakani na kuendelea, hususani tunapoelekea kwenye Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) nchini Azerbaijan mwishoni mwa mwaka huu.

Ni wazi kwamba zinahitajika fedha za kutosha, zaidi ya trilioni ya dola za kimarekani, kugharamia hasara na uharibifu, kuhimili, kukabiliana, na inabidi zitolewe katika utaratibu wa misaada na sio mikopo.

Hata hivyo ni vema ikafahamika vizuri kwamba hilo halitafikiwa kirahisi kutokana na mataifa tajiri kutokuwa tayari kuwajibika kwa matatizo waliyoyasababisha kwa zaidi ya karne sasa, hukwepa kujadili hali halisi na hupunguza viwango vya madhara, hujumuisha fedha yote inayokuja kwenye nchi masikini kama vile kupitia benki, mikopo na kwenye uwekezaji kuwa sehemu ya fedha hizo za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Zinafanyika pia jitihada na mataifa tajiri kupanua wigo wa wachangiaji wa uchafuzi wa hali ya hewa duniani ili nchi masikini zihusike pia kuchangia fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, na wanahakikisha unakuwepo uwekezaji zaidi kwenye kupunguza uzalishaji hewa chafu kwa manufaa ya mataifa tajiri kuliko kugharamia uharibifu na hasara na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi masikini.

Mataifa tajiri yamekuwa na kawaida kudai kuwa haiwezekani kuongeza kiwango cha fedha hizo za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, hata hivyo hesabu zilizofanywa na shirika la kimataifa la ActionAid inaonyesha mataifa hayo tajiri yana uwezo wa kuchangia dola za kimarekani trilioni mbili kwa mwaka kwa kupandisha viwango vya kodi kwa kampuni kubwa na matajiri.

Wakati watetei wa mazingira duniani wakipiga kelele kuhusu kutokuwepo usawa katika fedha za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi masikini, ni wajibu wa viongozi wa Afrika sasa kuchukua hatua za kukabiliana na huu mtego wa madeni yanayozalishwa kupitia fedha hizo.

Miongoni mwa njia zinazopendekezwa ili kufikia utenguzi wa mtego huo ni pamoja na suluhisho la kisiasa kwa wajumbe kutoka nchi za Kiafrika wanaoshiriki majadiliano katika mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 29), kutoachia maamuzi ya masuala muhimu yahusuyo mustakabali wa bara hili, kufanywa na nchi tajiri pekee ambao ndio wazalishaji wakuu wa hewa chafu duniani.

Kuhakikisha haki katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inatendeka kwa waathirika halisi, wananchi katika nchi masikini, badala ya kunufaisha wenye nguvu na mamlaka.

Mkurugenzi Mtendaji, Shirika la Kimataifa ActionAid, Kenya, Susan Otieno anachambua zaidi kuhusu suluhisho la mtego uliopo akisema, tafiti na mafunzo kuhusu Afrika yazingatie zaidi maarifa na maudhui yaliyo katika mukhtadha wa Afrika.

“Kuubomoa muundo wa mitego inayosababisha tupige hatua moja mbele na kisha kupiga hatua 10 nyuma,” anasema Susan.

Jambo lililo bayana hivi sasa ni kwamba nchi masikini, hususani kutoka Bara la Afrika, zinahitaji zaidi uwepo wa haki katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, na hili litawezekana tu pale viongozi na wajumbe katika meza za majadiliano wataposimamia maslahi ya bara hili.
 
View attachment 3105834

product (2).jpg
 
Back
Top Bottom