Cloatus Chama ana Ofisi Simba SC, si Young Africans

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
4,748
Reaction score
7,061
SIAMINI kabisa kama mpango wa Clatous Chota Chama kutoka Simba kwenda Young Africans una baraka za kocha Miguel Gamondi. Naamini hii ni mipango ya siasa zetu za kuoneshana ubabe, kuoneshana uwezo na kukerana.

Nikifuatilia suala hili naona mtazamo wa mashabiki wengi wa Simba ukibadilika kwa kasi ya ajabu. Walianza kutoa maneno makali kupinga kwamba Triple C asingeondoka Simba. Sasa naona wengi wanatoa kauli za kusisitiza mchezaji huyo aende tu, inawezekana kwa kukata tamaa au vinginevyo. Hii inaonesha kuwa jambo la kukerana linapoteza nguvu kwani waliokusudiwa kukereka wameanza kuonesha hawakereki.

Inawezekana nguvu kubwa ya kumtaka Chama Young Africans zaidi ni ya kupata faida nyingine na wala si mchango wa mchezaji huyo kwa timu. Kuna faida za kibiashara ya jezi, watu kulipa na kufurika uwanjani siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi na pia viongozi wa Young Africans kuongeza hali ya kupendwa na kuaminiwa na mashabiki lakini kiuchezaji, siioni ofisi ya Triple C Young Africans ikizingatiwa kocha Gamondi mwenye msimamo mkali na asiyeingiliwa na uongozi, tayari ameshawagawia ofisi wachezaji wake alionao sasa na tayari wanatia mzigo vizuri kulingana na falsafa ya uchezaji wa Young Africans.

Palipo na Muddathir Yahya, Pacome Zouzoua, Max Nzengeli na Stephen Ki Aziz ukimtaja pia Khalid Aucho unahitaji nini zaidi? Nani miongoni mwa hawa ajiunge na Salum Abubakar Salum, Zawadi Mauya na Shekhan Khamis ukimtaja pia Jonas Mkude kukaa bench ili Mwamba wa Lusaka apate ofisi ya kudumu Young Africans?

Hoja itatolewa kuwa timu kubwa huwa na wachezaji bora wengi wa nafasi moja ili kuifanya timu iwe imara nyakati zote kwa kutokosa mchezaji mzuri mabadiliko yakifanywa, dharura mbalimbali zikitokea na kukabili mashindano mengi. Kutekeleza hilo palihitajika, kwa pesa inayohusu biashara ya Clatous Chota Chama, angetafutwa mjuzi mno, mwenye kasi iendayo na falsafa ya uchezaji wa Young Africans atakayedumu kwa misimu kadhaa au atakayeuzwa kwa faida kubwa lakini kuingia gharama kubwa hivyo kwa Chama aliyevuka umri wa miaka 30 kulipaswa kufanyiwa tafakari ya kina.

Tunaambiwa timu hununua wachezaji wajuzi wa umri mkubwa kufanikisha malengo ya muda mfupi lakini Young Africans wameshafika fainali Afrika, wamefika robo fainali Afrika na wamechukua ubingwa wa Tanzania Bara mara tatu mfululizo na CRDB Shirikisho. Siamini wanahitaji mchezaji wa umri mkubwa wa uchezaji wa taratibu wa Chama kufanikisha lolote la sasa. Akili yao ilipaswa, kwa kutumia pesa ya kumpata Chama, iwaelekeze kufukua sehemu mbalimbali Afrika na kumpata mchezaji kijana mwenye kasi kama ilivyotokea kwa Ki Aziz ili awasaidie kwa mengi kwa muda mrefu.

Nionavyo kama Young Africans itafanikiwa kumpata Triple C kutoka Simba, Simba watanufaika zaidi ya Young Africans. Hii ni kwa sababu Simba walishampa mchezaji huyo ofisi ya kudumu na alikuwa mfalme. Hawakuwa wakifikiri kutafuta wachezaji wengine bora wa nafasi yake kutokana na ufalme waliompa. Ninachoona kwa sasa ni kama Simba watakuwa wameondolewa mzigo huo na hivyo watatafuta wachezaji wajuzi wa umri wa miaka 20 na kadhaa kuikamata ofisi hiyo. Kwa ufalme wake, Simba wasingempa 'Thank You' kirahisi kama walivyofanya kwa wengine. Pia wasingefanya hivyo kukwepa lawama kutoka kwa mashabiki wao kwani walijua 'Thank You' yao ya hapo Kariakoo ingepokelewa mara moja na 'Welcome' ya upande mwingine wa hapo hapo Kariakoo.

Kwa upande wake, Chama, atakuwa amefaulu kufanikisha kupata pesa kubwa ya malipo ya kusaini mkataba na mshahara mkubwa wa mwezi. Kwa hayo anastahili pongezi kwani hayo ni maisha yake na kila mtu ana maisha yake kipekee. Mwamba wa Lusaka anajua vizuri kuliko sisi wengine kwamba ajira ya soka ni ya muda mfupi kuliko ajira zote. Hivyo ukipata fursa ya kukusanya pesa nyingi kwa muda fulani mfupi ndani ya kazi ya soka, usiitupe fursa hiyo.

Kwa Young Africans, wao watafanikisha malengo yoyote mengine lakini mchango wa mchezaji huyo kwao naamini hautakuwa mkubwa. Ataingia ofisi ya nani? Max? Pacome? Ki Aziz? Muddathir? Au atapewa jukumu jipya? Je atachangamka kuendana na uchangamfu wa Young Africans?

Simba watateseka kwa kuzomewa na kubezwa lakini watakuwa wamepata fursa ya kuingiza vipaji vipya ndani ya ofisi ya Mwamba wa Lusaka. Kwa uhakika mwamba huyo ana ofisi ya uhakika Simba lakini hana uhakika wa ofisi Young Africans. Akifanikiwa kwenda huko, utabaki wajibu wake kupambana kuishi kama mchezaji wa Young Africans akienda na mapigo ya muziki wao.

Vyovyote atakavyoamua kuhusu wapi afanye kazi msimu huu, uamuzi wa mchezaji huyo unapaswa uheshimiwe kwani atakuwa ameamua atakavyoamua kwa kujali maisha yake na si maisha yetu sisi wengine. Kila mtu ana maisha yake na anapanga afanye yapi kuyafanya yampe furaha, amani na afya nzuri. Tumuache Triple C na maisha yake.

Baada ya utumishi wake wa mkataba atakaoingia sasa kokote kule hapo Kariakoo, ni vizuri aweke mkakati kichwani wa kurudi nyumbani Zambia kwenda kumalizia huko kucheza soka. Kwake kufanya kazi Tanzania kutakuwa kumetosha. Ameishi muda mrefu kama mfalme asimalize kama mtu wa kawaida huko Singida Black Stars au Coastal Union. Tuheshimu uamuzi wowote wa sasa hivi wa Mwamba wa Lusaka.
---UZI HUU, NIMEUTOA FACEBOOK, UMEANDIKWA NA BW. IBRAHIM MKAMBA.
Nimevutiwa kuuleta huku, baada ya 'kufikiri' kuwa una VIWANGO vya hapa JF.
 
Yanga kwa hivi karibuni ilikuwa imeshaondokana tabia ya wachezaji wanaojivuna, wanaopenda ufalme na umwamba (mafaza) kumleta Chama ni kurudi kule kule nyuma ambako huwa ni mwiko. Chama ni aina ya wachezaji wasumbufu wanaopenda kuwa mtawala. Ukiangalia kwasasa Yanga ina ma star haswa kama Pacome, Aziz Ki, Max, Diarra na Yao lakini hawa wanajiona sio kitu bila uwepo wa wachezaji wenzao. Wamedumisha ushirikiano na umoja kama timu na hakuna hata mmoja aliyeonesha yeye ndio kila kitu. Angalia namna Azizi Ki pamoja na kuimbwa sana lakini amekuwa na upendo na kujali zaidi wenzie na kutamani wenzie wang'ae zaidi. Hakuna mabifu ya wachezaji kwa wachezaji pale Yanga na ndio maana unaona Lomalisa yupo benchi ila ikitokea tukio la kushangilia sio ajabu kumuona akikumbatiana na mshindani wake kinafasi (Kibabage) hakuna ufalme kwenye timu ya Yanga.

Napata wasiwasi kama ujio wa Chama utaweza ku maintain umoja na ushirikiano wa timu kama awali?

Kwenye upande wa kiufundi, Chama wa sasa kwavile umri umeenda na jinsi anavyojilinda kwavile kabakiza safari fupi kwenye ulimwengu wa soka amekuwa na changamoto ya kasi na pia hapendi mipira ya kugongana au ile ya 50 kwa 50 kugombaniana labda kwavile kuna watu wengi wa kazi labda kocha ataamua kumtumia kwa kumpunguzia majukumu au vile yeye kocha anaona inafaa Ila kwa mpira wa Gamondi hawezi kutekeleza majukumu yote ( kukaba na kupoka mipira, na kushambulia kwa kasi)
 
Ni vile tu sina mamlaka ya kusajili. Ila kama ningekuwa nayo; hakika ningetafuta mchezaji mwenye kipaji kikubwa na pia mwenye umri mdogo kuliko huyo Chama.

Kwa Prince Dube, ✔️
Huyu amesajiliwa kisiasa za soka la bongo tu na siyo kuwa atakuwa na kitu kikubwa cha ku offer Yanga.
 
Huyu amesajiliwa kisiasa za soka la bongo tu na siyo kuwa atakuwa na kitu kikubwa cha ku offer Yanga.
Asipokuwa makini, na yeye ataishia tu kuwa kama mwenzake Skudu Makudubela. Yaani alisajiliwa kwa ajili ya burudani, na siyo kuiletea timu mafanikio kama walivyofanya akina Aziz Kii, na wengineo.
 
Mimi shabiki wa Yanga, lakini, kwa CCC hapo hakuna mchezaji. Kiwango chake ni kidogo ukilinganisha na ubora wa Yanga.

Kama kweli Yanga watamchukua Chama, basi watakuwa wamemchukua kwa sababu za "siasa ya mpira" na siyo sababu za kiufundi.
 
Mimi shabiki wa Yanga, lakini, kwa CCC hapo hakuna mchezaji. Kiwango chake ni kidogo ukilinganisha na ubora wa Yanga.

Kama kweli Yanga watamchukua Chama, basi watakuwa wamemchukua kwa sababu za "siasa ya mpira" na siyo sababu za kiufundi.
Mkuu siyo kama watamchukua, amesha sajiliwa tena kwa donge nono.

Ukilinganisha na kiwango chake cha sasa, anasubiria utambulisho tu.
 
okrah alivimba bench , gwede alikuja kavimba akapoa, chama akizingua December tu wanamtoa mkopo. aziz ki alivimba few days akaambiwa kama anataka kusepa asepe. star yanga ni diara.
 
Unapaswa kulithibitisha hili kwa wewe kuleta link hapa. Kwasababu wewe umelileta hilo jambo humu kwenye JF sio YouTube. Onesha hapa kwa kuweka link
ambaye ujui ni wewe tu. why should I bother??
upo nyuma nenda kaji update habari zipo.
 
ambaye ujui ni wewe tu. why should I bother??
upo nyuma nenda kaji update habari zipo.
Ulijua humu Facebook kuropoka bila kuulizwa uthibitisho na ushahidi? Pole humu sio kijiwe cha umbea usio na vielelezo. Siku nyingi ujifunze kutofautisha kati ya jamii forum na Facebook. Ukiambiwa ulete uthibitisho usiingie mitini kwa ngonjera. Hapa ni mwendo wa kujibizana kwa hoja na vielelezo halisi.
 
it's a simple instruction. Just use you tube ffs.
is that hard for you??
Acha kutafuniwa kila kitu. tafuta vitu.
 
Guede, Okrah na Aziz Ki uliona wapi wakivimba? Nikumbushe ni tukio lipi lilionesha kuwa wamevimba?
Utakuwa mgeni na huyo jamaa.. huyo anaongoza humu kwa unafiki, uongo, uzushi na maneno ya kimbea kama mtoto wa kike. Huyo kuna nyuzi alileta kuwa Guede anamuhonga Gamondi ili acheze. Kuna vinyuzi kibao kaleta kushinikiza uongozi wa Yanga umtimue Gamondi... Na alisema ana uhakika jumatano Gamondi anatangazwa na Kaizer chief kuwa kocha mkuu. Miongoni mwa watu niliotokea kumdharau ni huyu jamaa mzushi...
 
Umeongea ukweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…