Cloatus Chota Chama anataka mpunga mrefu ili kubaki Simba

Cloatus Chota Chama anataka mpunga mrefu ili kubaki Simba

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
1719346021169.png

Cloatus Chota Chama

Ni kweli bado hakijaeleweka. Kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama bado hajamwaga saini ya kuendelea kubali Simba baada ya mabosi wa Msimbazi kushindwa kumtekelezea mahitaji aliyowasilisha mezani ili asalie kikosini.

Ipo hivi. Utata umeibuka ni baada ya mabosi wa Simba kugomea kumuongezea ada ya usajili (sign on fee) ambayo kiungo huyo alikuwa anaitaka ili asaini mkataba wa kuendelea kusalia katika timu hiyo. Simba ni kama imeingia nyongo na Chama ambapo baadhi ya mabosi ndani ya klabu hiyo wakiona Mzambia huyo bado anahitajika, huku kundi lingine lenye nguvu likiona ni bora watengeneze timu mpya itakayokuwa bila ya mchezaji huyo.

Hatua ya pili ambayo Chama na Simba inabishana ni juu ya mshahara ambao anautaka ambao ni sawa au zaidi na ule anaolipwa sasa winga Luis Miquissone. Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, mabosi wa Simba na Chama wameshindwa kuafikiana kwenye dau hilo la mshahara, kwani Mzambia huyo ametaka kulipwa Dola 20,000 (Sh 52 milioni) kwa mwezi.

Kwa sasa inadaiwa, Luis Miquissone ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza au kupata nafasi ya kutumika mara kwa mara kikosini, analipwa na Simba zaidi ya Dola 17,000 (Sh 44 milioni) kwa mwezi, mshahara ambao Chama ametaka zaidi ya kiwango hicho ili asaini mkataba mpya na mabosi wa Simba wanaona ni vigumu kumkubalia.

Hatua ya mwisho kwa Simba ni kama kundi linalotaka Chama aachwe linaelekea kushinda kwa vile wao ndio wanaotoa uamuzi makubwa ya bajeti ya klabu hiyo.

PIA SOMA

- Nini Chama? Kulikuwa na Emmanuel Anorld Okwi, Nteze John Lungu na wengineo!
 
Tutaongezea vyura kwny huo mfumuko ili tupate upya mzuri...
Mkiongeza vyura, hapo mnakuwa hamjafumuliwa bali mmeongeza. Inatakiwa mfumuliwe na mashabiki wote ili wawe wapya kama ilivyo kwa timu na jezi itakavyofumuliwa.
 
mashabiki wanahusu nini kwmy benchi la ufundi...wawe wapya...wengineunataka waje kushangilia utopolo au?
Samahani mkuu, hivi hapo kwenye utopolo ndio timu ipi hiyo? Au ndio ile inayocheza klabu bingwa msimu ujao kwa tiketi ya bingwa wa Tanzania? Samahani kwa maswali lakini, ningependa tu kujua
 
Samahani mkuu, hivi hapo kwenye utopolo ndio timu ipi hiyo? Au ndio ile inayocheza klabu msimu ujao kwa tiketi ya bingwa wa Tanzania? Samahani kwa maswali lakini, ningependa tu kujua
Ingia gugo...
Utopolo...
Makolo...
zote zipo haijalishi inacheza ligi ipi..
 
Mbona kama umepanick? Jezi ni kionjo tuu kwny habari..the main content hapo ni timu ifumuliwe...
Hapana siwezi kupaniki kwasababu mimi sio mwana shirikisho wala mwana muungano, mimi ni bingwa anayeenda kupambana na mabingwa wenzake.

Content ni mabadiliko ya timu, na timu huenda sambamba na mashabiki. Sasa kama mashabiki wanafurahia kuletewa Manzoki kwenye mkutano, kama mashabiki wanaambiwa kibegi na Whatsapp channel ni mafanikio kisha wanafurahia, shabiki anaridhika hadi na kombe la kisiasa la muungano hao nao wanastahili kufumuliwa waje mashabiki wanaojitambua na viongozi wakajua kuna watu timamu hivyo hatupaswi kufanya blah blah tena.
 
Hapana siwezi kupaniki kwasababu mimi sio mwana shirikisho wala mwana muungano, mimi ni bingwa anayeenda kupambana na mabingwa wenzake...
Tupisheee...pambana na timu yako ya huku yaache...kwny club hukosi kila aina ya watu...huwezi tenganisha timu na mashabiki.

Huko unakojitapa tumekuwepo for 5 good years kwa kujirudia..kaaa kwa kutulia huko kwenu..mashabiki wa Simba hawakuhusu...huna haja ya kukauka mate kisa mboga ya jirani inaungua..
 
Ni kweli bado hakijaeleweka. Kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama bado hajamwaga saini ya kuendelea kubali Simba baada ya mabosi wa Msimbazi kushindwa kumtekelezea mahitaji aliyowasilisha mezani ili asalie kikosini...
Aende tu
 
Tupisheee...pambana na timu yako ya huku yaache...kwny club hukosi kila aina ya watu...huwezi tenganisha timu na mashabiki...huko unakojitapa tumekuwepo for 5 good years kwa kujirudia..kaaa kwa kutulia huko kwenu..mashabiki wa Simba hawakuhusu...huna haja ya kukauka mate kisa mboga ya jirani inaungua..
Mboga ya jirani imeungua kisa kwenda kushabikia ugomvi usiomuhusu na kujisahau kama anapika. UBUTHU BOTHO 😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom