Clouds 360 yawauliza Bodaboda kama Mbowe alivamiwa au alianguka mwenyewe jijini Dodoma

Clouds 360 yawauliza Bodaboda kama Mbowe alivamiwa au alianguka mwenyewe jijini Dodoma

Hao 360 kweli wapuuzi, unawauliza bodaboda kuhusu Mbowe kwani walikuwepo kwenye tukio? na wanavyosema "kwa unavyomfahamu" kwani hao boda wanaishi na Mbowe?! au kumfahamu kwa kumtazama kwenye Tv!.

Maana yake kuna jibu walikuwa wanategemea kupewa, bahati mbaya kwao bodaboda wameonesha "professionalism" zaidi ya hao waandishi makanjanja.
 
Watangazaji wa Clouds 360 wametembelea kijiwe maarufu cha kahawa jijini Dodoma na kufanya mahojiano na madereva wa Bodaboda.

Bodaboda waliulizwa maswali mawili ya msingi:

1. Je, Rais Magufuli akimaliza muhula wake wa pili wa uongozi aongezewe 10 mingine?

2 Je, kwa mnavyofahamu Mwenyekiti wa CHADEMA mh Mbowe alivamiwa au alianguka mwenyewe?

Bodaboda wamependekeza Rais Magufuli aendelee na uongozi hadi maono yake yatakapokamilika.

Kuhusu Mbowe bodaboda wamesema wao hawajui chochote na walitegemea waandishi wa habari ndio wenye taarifa zaidi.

Source Clouds tv

Maendeleo hayana vyama!
Konokono
 
Badala kuwahoji wabobezi wa masuala ya kitaifa kuhusiana na mambo ya msingi, wao wanakimbilia kwenye makundi ambayo watapata kiki za kirahisi. Huku ni kujidharaurisha tu.
Akili hizo za kuhoji wabobezi wanazo sasa!?
Wao uwezo wao kiakili ndio huo wa mambo yaongelewayo kwenye vijiwe vya kahawa,bodaboda na "red light district".
 
Watu wapo kikazi hapo...tumbo kwanza mengine baadae.
 
Hao 360 kweli wapuuzi, unawauliza bodaboda kuhusu Mbowe kwani walikuwepo kwenye tukio? na wanavyosema "kwa unavyomfahamu" kwani hao boda wanaishi na Mbowe?! au kumfahamu kwa kumtazama kwenye Tv!.

Maana yake kuna jibu walikuwa wanategemea kupewa, bahati mbaya kwao bodaboda wameonesha "professionalism" zaidi ya hao waandishi makanjanja.
Tatizo wanawauliza wasiohusika. Mnyika alisema Mbowe hakuwa peke yake. Waandishi wamfuate Mnyika awatajie watu walikuwa na Mbowe halafu wafanye mahojiano nao.
Kwanini hao watu hawatajwi? Au nao ni wasiojulikana?
 
Hao 360 kweli wapuuzi, unawauliza bodaboda kuhusu Mbowe kwani walikuwepo kwenye tukio? na wanavyosema "kwa unavyomfahamu" kwani hao boda wanaishi na Mbowe?! au kumfahamu kwa kumtazama kwenye Tv!.

Maana yake kuna jibu walikuwa wanategemea kupewa, bahati mbaya kwao bodaboda wameonesha "professionalism" zaidi ya hao waandishi makanjanja.
Kiongozi mkui mmoja kuotaja Clouds inamshinda anasema klaudi
 
Badala kuwahoji wabobezi wa masuala ya kitaifa kuhusiana na mambo ya msingi, wao wanakimbilia kwenye makundi ambayo watapata kiki za kirahisi. Huku ni kujidharaurisha tu.
Makundi hayo waliyoyahoji pia yana nafasi yao katika jamii ya Watanzania na wanazo haki zote za kiraia ila kilichoniboa ni kuwauliza issue ya Mbowe kana kwamba ama wakati anavamiwa na kupigwa au wakati anadondoka kwa ulevi wa Faru John walikuwepo
 
Hivi boda boda hapa anausikaje? Akuwepo kwenye tukio, hana mamlaka ya kufanya uchunguzi, majukumu yake ni tofauti na matukio hayo.
Waulize majirani zake, polisi,mzazi mwenzie, dereva wake, baa alikokunywa kama kweli, madaktari waliomuhudumia.
Maana inafikirisha kidogo maelezo mbalimbali, kuumia kwa kupata jeraha la kuanguka, au kuumia kupata jeraha la kupondwa pondwa.
Pia ujuwe mchicha unaandaliwa kwa kukatwa katwa, ila kisamvu uandaliwa kwa kupondwa pondwa, hivyo ujue jeraha lilikiwa na hali gani, ukijuwa tu unaweza usimuhoji mtu!
 
Back
Top Bottom