Clouds 360 yawauliza Bodaboda kama Mbowe alivamiwa au alianguka mwenyewe jijini Dodoma

Hao 360 kweli wapuuzi, unawauliza bodaboda kuhusu Mbowe kwani walikuwepo kwenye tukio? na wanavyosema "kwa unavyomfahamu" kwani hao boda wanaishi na Mbowe?! au kumfahamu kwa kumtazama kwenye Tv!.

Maana yake kuna jibu walikuwa wanategemea kupewa, bahati mbaya kwao bodaboda wameonesha "professionalism" zaidi ya hao waandishi makanjanja.
 
Konokono
 
Badala kuwahoji wabobezi wa masuala ya kitaifa kuhusiana na mambo ya msingi, wao wanakimbilia kwenye makundi ambayo watapata kiki za kirahisi. Huku ni kujidharaurisha tu.
Akili hizo za kuhoji wabobezi wanazo sasa!?
Wao uwezo wao kiakili ndio huo wa mambo yaongelewayo kwenye vijiwe vya kahawa,bodaboda na "red light district".
 
Watu wapo kikazi hapo...tumbo kwanza mengine baadae.
 
Tatizo wanawauliza wasiohusika. Mnyika alisema Mbowe hakuwa peke yake. Waandishi wamfuate Mnyika awatajie watu walikuwa na Mbowe halafu wafanye mahojiano nao.
Kwanini hao watu hawatajwi? Au nao ni wasiojulikana?
 
Kiongozi mkui mmoja kuotaja Clouds inamshinda anasema klaudi
 
Badala kuwahoji wabobezi wa masuala ya kitaifa kuhusiana na mambo ya msingi, wao wanakimbilia kwenye makundi ambayo watapata kiki za kirahisi. Huku ni kujidharaurisha tu.
Makundi hayo waliyoyahoji pia yana nafasi yao katika jamii ya Watanzania na wanazo haki zote za kiraia ila kilichoniboa ni kuwauliza issue ya Mbowe kana kwamba ama wakati anavamiwa na kupigwa au wakati anadondoka kwa ulevi wa Faru John walikuwepo
 
Hivi boda boda hapa anausikaje? Akuwepo kwenye tukio, hana mamlaka ya kufanya uchunguzi, majukumu yake ni tofauti na matukio hayo.
Waulize majirani zake, polisi,mzazi mwenzie, dereva wake, baa alikokunywa kama kweli, madaktari waliomuhudumia.
Maana inafikirisha kidogo maelezo mbalimbali, kuumia kwa kupata jeraha la kuanguka, au kuumia kupata jeraha la kupondwa pondwa.
Pia ujuwe mchicha unaandaliwa kwa kukatwa katwa, ila kisamvu uandaliwa kwa kupondwa pondwa, hivyo ujue jeraha lilikiwa na hali gani, ukijuwa tu unaweza usimuhoji mtu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…