Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu mmoja, Mwijaku unatumja kama mfano wa kuisema clouds imekosa Ladha. Una conflict of Interest. Zama zinabadilika kama umezeeka we tulia, sisi generation yetu tunaenjoy kina mwijaku we usilazimishe tupende ladha za generation zako.
Ata bongo fleva ya zamani sio ya leo bongo fleva ya sasa imetawaliwa na Mapiano.
Aina ya mziki nadhani nasikia tu wanasema mapiano sijui amapiano, ila nilichokuwa najaribu kuelezea ni kwamba mambo yanabadilika, yaliyofanyika 2010 hayawez fanana na ya mwaka 2023 sasa ww kama unataka yawe kama ya 2010 rudi uko 2010 ukawasikilize kina ephraim kibonde sasa tuache sisi tunaoenda na upepo uliopo tuende nao ivo ivo.Mapiano ndio nini kiongozi...?
RFA na Kiss walikuwa strong sanaWakati naskiliza KISS FM na RFA walikuwa na vipindi vizuri tu sjui kwa sasa hivi.
Hio station sana sana ni kwa ajili ya vijana hata kipindi hicho ni mara chache sana kumkuta mtu mzima akisiliza kutokana na contents zakeMuda wa kupoteza uelekeo au...?
Aina ya mziki nadhani nasikia tu wanasema mapiano sijui amapiano, ila nilichokuwa najaribu kuelezea ni kwamba mambo yanabadilika, yaliyofanyika 2010 hayawez fanana na ya mwaka 2023 sasa ww kama unataka yawe kama ya 2010 rudi uko 2010 ukawasikilize kina ephraim kibonde sasa tuache sisi tunaoenda na upepo uliopo tuende nao ivo ivo.
Zamani iyo ulikuwa uwez sikiliza vipindi vya radio radio kuiptia YouTube na hata tulikuwa hatujui uko studio kunafananaje ila saiv vipind wanastream Youtube tunaona hadi studio wanachokifanya wewe kama ushazeeka kubali uzee ndugu
Hio station sana sana ni kwa ajili ya vijana hata kipindi hicho ni mara chache sana kumkuta mtu mzima akisiliza kutokana na contents zake
FM radio stations za Tz nadhani hazina Program manager, anaweza kuwa anaongea mgeni ghafla Tangazo likaingia
RFA ilikua balaa mkuuOngeeni yote ila hakuna radio iliyokuwa na quality kama Kiss Fm na RFA
Leotena na Dina MariosSALAAM...!
Natumai muwazima kabisa. Well...!
Clouds FM (CMG) ni Radio iliyoleta mapinduzi katika huu muziki wa kizazi kipya na hata miziki mingine, tangu ilivyosemwa kuwa muziki wa Bongo Flavor ni uhuni watu waliukataa. Ila niseme tu, ujio wa radio hii uliwaaminisha WENGI sana kuwa huu muziki sio uhuni na wala sio muziki wa wahuni hata kidogo, japo matendo ya wanamuziki hao yalionekana ni ya kihuni.
Kipindi hiko tukiskiliza Clouds FM tuliskia sauti za kina Bony Love (DJ BONNY) na K-Single (KIBACHA) Wa Kwanza Unit (K-U Crew) katika Daktari wa Midundo (DR. BEAT) kabla hatujaamshwa na FINA MANGO, MASOUD KIPANYA na GERALD HANDO,bila ya kumsahau BARBARA HASSAN katika POWER BREAKFAST.
Tuliendelea kuburudishwa na Dada Mkuu AMINA wa CHIFUPA A.K.A (AMINA MPAKANJIA) akiwa na ZAMARADI MKETEMA na GEAH HABIB katika (LEO TENA) huku JAHAZI likiongozwa na CAPTAIN GADNER G HABASH kabla ya kuingia OTHAMN NJAIDI kutoka MAWINGU BAND na Bugigo (DJ BOOGY MASTER) kwenye AFRICA BAMBATAA. Usiseme nimemuweka pembeni DJ SKILLZ na DJ MOOLY BLING BLING ( MOOLY B) ila kaa ukijua tu kuwa tunathamini michango yao. Bila ya kumsahau LADY JD.
Mdogo mdogo tulimalizia show na DJ BONNY LOVE bila ya kumsahau mdogo wake DJ BONNY VENTURE na mwisho wakitukabidhi FINA MANGO tulale nae mpaka mida mibovu baada ya kumaliza na EPHRAIM KIBONDE kwenye kipindi chake cha michezo akiwa na CYPRIAN MUSIBA au MUSIBA CYPRIAN kama skosei hata skumbuki aisee, usiku m-bovu tukiwa na DJ ELLY huku SEBASTIAN NDEGE akituliwaza na story zake za MATUMAINI kila JUMAPILI wakati Kaka BONDA akitulelea watoto wetu kila JUMAMOSI asubuhi kabla hajaingia K-SINGLE na BONNY kwenye kipindi cha BONGO FLAVA.
Lakini leo hii, siipati ile ladha ya Clouds kama Clouds niliyoizoea before. Clouds ya leo ina wakina Mwijaku...! KWELI...?
Hao wakina Babuu, Jose Mara, Kennedy na wengine siwajui nawaskia tu, therefore sina comments zao kihiiivyo coz imekuwa ngumu kuskiliza Clouds kama nilivyokuwa naskiliza zamani coz 'FLAVA'/'LADHA' niliyokuwa naipata mwanzo siipati tena.
Hivi kweli leo hii Clouds FM kama Radio Kongwe Tanzania inaajiri mtu kama Mwijaku, KWELI...? ILI IWEJE...?
Kwenye LOOPHOLE unawapa watu nafasi ya kupenya na wakishapenya inakuwa NGUMU sana kuwarudisha walipotoka. Hatukatai sawa biashara ni matangazo, ila SERIOUSNESS ndio KILA KITU. SIO UKATUNI..! SIO UTANI...!.
RUGE amekufa akiwa ameiacha Radio kwenye status nzuri sana, ila status ambayo ameiacha RUGE ukilinganisha na sasa siwezi ku-judge wala ku-compare. Lazma ukweli usemwe, kuna mtu kama Adam Mchomvu amefanya ujinga mwingi sana Clouds huku BIG JOE akimuangalia tu, siwezi juwa wana uhusiano gani na wala staki kujua ila, Brand itabaki kuwa ni brand tu daima milele.
Kwangu mimi afadhali ya ADAM kuliko huyu jamaa ambaye niliuliza, hivi huyu ni nani, watu wakaniambia ni mtangazaji wa Clouds FM. Nikabaki nashangaa, hivi ni kweli Clouds iliyokuwa inaibua watangazaji wanaojilelewa leo hii inaajiri watu wa aina hii, KWELI...?
Sina cha kulaumu wala kushauri ila nimebaki nikiwaza tu ilivyokuwa CLOUDS FM | BEFORE & AFTER.
NDIVYO ILIVYOTAKIWA KUWA SASA HIVI ILIVYO CLOUDS FM...?
KWELI...?
KIND REGARDS.
View attachment 2677774