Clouds FM na Millard Ayo nani anamtegemea mwenzake?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Mabadiliko ya vipindi vya Redio yamekiondoa kipindi cha Amplifier, kutoka kwenye studio za CMG na muda wake uliozoeleka kutoka saa 1: 00 (usiku) hadi saa 3 : 00 (usiku) kwasasa kinarushwa studio Millardayo Blogspot (Palm village) kuanzia saa 10 jioni hadi 1 usiku.

Swali langu:

Je! kati ya Clouds Media Group na Millardayo Blogspot nani anamtegemea mwenzake katika kutimiza wajibu? Yaani Kipindi cha Amplifier hakiwezi kwenda hewani bila Mtangazaji wake Millard Ayo na Millardayo Blogspot haiwezi kujitangaza bila Millard Ayo kutangaza.
 
Kuna kitu kinaitwa interdependent ndo kilichopo Kati ya clouds na millard yaan hakuna anayemtegemea mwenzake na kanuni ya kwanza ya interdependence ni lazima kila anayeshiriki awe independent(yaan awe na uwezo wa kufanya shughuli zake bila utegemezi)

So Millard anaweza kuacha kipind na clouds wanaweza kuishi bila Millard na maisha yakaendelea vizuri tu kwa sababu kila mmoja ni independent na siyo dependents kwa mwingine.
 
Acha kulinganisha mtu na taasisi mkuu...

Nadhani bila clouds millard asingekuwa ivyo leo, coz aliwahi kuwa katika vyombo vingine ila akupata chachu kama aliyopata clouds!

Japo anajiweza kwa kila kitu jiulize... kwanin ajasepa kabisa kama anahisi ana uhitaji na clouds..!
 
Clouds na hii kampeni yao ya Shangazi Big sijui nini hata siwaelewi wanavuruga vuruga vipindi pasi na mpangilio..

Kuna kila dalili naona Millard atahama media na kuondoka kabisa CMG, japo ina mchango mkubwa katika career yake

Sent from my SM-J720F using JamiiForums mobile app
 
Ila wengine Tena wengi tu wanawaelewa.
 
Binafsi namjua Millard Ayo Wa Clouds, Nje ya Clouds huyu Jamaa simjui kabisa..

So, nionavyo Mimi; Millard Ayo bila Clouds ataathirika kwa namna moja ama nyingine. Ilhali Clouds bila Millard sidhani kama itaathirika kivyovyote vile.
 
Binafsi namjua Millard Ayo Wa Clouds, Nje ya Clouds huyu Jamaa simjui kabisa..

So, nionavyo Mimi; Millard Ayo bila Clouds ataathirika kwa namna moja ama nyingine. Ilhali Clouds bila Millard sidhani kama itaathirika kivyovyote vile.
Millard huyu huyu ambaye taifa zima linategemea page yake ya insta kama chombo kikuu cha habar??mwenye subscribers wa kutosha huko you tube??

Sababu pekee inayomuweka pale clouds ni kwamba anawaheshimu na ilikuwa dream yake kufanya kazi clouds

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clous n kubwa kuliko millard jmn ,millard ndio tegemezi kwa clous achen masihara.
 
Marehemu Ruge alikuaga mafia alikua anaonaga mbali sana linapokuja swala la chapaa
Wakati Ayo anaanza kutrend sana kwenye digital platform CMG walimbana ikabidi akaisajili “Milard Ayo” na CMG ni mbia
So Ayo pale CMG ni zaidi ya muajiriwa lakini ana ubia na CMG kwenye digital platform zake
 
Binafsi namjua Millard Ayo Wa Clouds, Nje ya Clouds huyu Jamaa simjui kabisa..

So, nionavyo Mimi; Millard Ayo bila Clouds ataathirika kwa namna moja ama nyingine. Ilhali Clouds bila Millard sidhani kama itaathirika kivyovyote vile.
Mtu huzaliwa, hutambaa, hutembea ,Lukas na hatimaye hujitegrmea.
Sijui kwa nini huu ukweli mnaukwepa!

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi kote huko sijawahi kumfuatilia, zaidi huwa namsikia kupitia Clouds pekee..
 
Jamani nimekumbuka Shule ya msingi, nilimwandikia demu barua kumbe hajui kusoma. Yaani tumesimama mstarini, naiona barua yangu hiyo inapeperuka
 
Millard Ayo blogspot ndio nini?

Ok ngoja tuende hivyo kuhusu nani anamtegemea mwenzie bila shaka wote wanategemeana na millard anategemea zaidi clouds sababu ndio imemfanya awe lakini pia huenda kipindi cha amplifaya ni kipindi cha millard hivyo clouds inampa airtime ili kipindi chake kuruka (nimesema huenda).
Lakini swala kubwa hapo ni mkataba wao unasemaje. Lakini pia swala la kipindi kubadilishwa kutoka saa 1 na kurudishwa saa 10 Huenda kunasababu nyingi mfano wanaweza kuangalia swala la washindani wakati wa kipindi hicho mfano muda kilipokuwa kikiruka kwa hewa kipindi hicho hata Efm kuna kipindi cha empire cha Jonijooo, dj spaa na Bdozen B12 twagala hivyo baadhi ya watu hawakusikiliza amplifaya na hivyo kusikiliza empire kwahiyo wanaweza fanya hivyo kwa kuangalia washindani wake.

Pia millard kipindi hicho huruka nacho akiwa sehemu mbalimbali anaweza kuwa studio za clouds, maeneo mengine Dar na nje ya dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…