Clouds FM warusha kisa cha kushtua!!

Clouds FM warusha kisa cha kushtua!!

Yo Yo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Posts
11,210
Reaction score
1,720
460%3E_1984865.jpg


[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-22T06_43_14-07_00.mp3[/mp3]


Vipindi vingine hivi:

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-23T05_32_36-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-21T05_23_18-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-20T06_46_25-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-17T06_29_25-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-16T06_11_40-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-15T05_38_03-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-15T05_24_18-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-13T05_52_37-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-10T05_08_35-07_00.mp3[/mp3]

[mp3]http://hekaheka.podomatic.com/enclosure/2009-07-09T06_11_58-07_00.mp3[/mp3]
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji na waandishi wengine,

Hawa POLISI na huyo kijana wanatakiwa WAISHIE KEKO. Kitendo cha kumaliza kesi kisirisiri inabidi kweli hii wachukuliwe hatua kali sanaa. Hawa akina dada inabidi hii kesi waivalie njuga. Ikibidi magazeti mengine na TV basi lifuatilieni hili.....

Ningelikuwa ni mimi, ningelifanya alichofanya Samuel L. Jackson kwenye ile film ('A Time to Kill'). Ningelimsaka hadi nimpate hapohapo kwenye duka lake la kutengeneza simu na siku hiyo huyo Muhamed Kibaka angelikiona cha moto.

Hii ntakuwa naingia kuilaani kila siku kwa siku tano.
 
Last edited:
Waungwana naomba msaada wenu wa namba za simu zifuatazo;

1. Kituo cha Redio cha Clouds.(Majina halisi ya Watangazaji wa kipindi kilichorusha
matangazo ya uzalilishwaji wa Watoto wa kike)

2. Namba ya simu ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke.

3. Namba ya simu ya Kituo cha Polisi Mgulani/Kilwa Road.

4. Namba ya simu ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mgulani.

Mkuu Yo-Yo naomba utafute muda ili urushe tena majadiliano ya pili ya wadada hao ambayo yatafanyika kesho kwa mujibu wa Matangazo ya hao Clouds...
 
Mwanakijiji na waandishi wengine,

Hawa POLISI na huyo kijana wanatakiwa WAISHIE KEKO. Kitendo cha kumaliza kesi kisirisiri inabidi kweli hii wachukuliwe hatua kali sanaa. Hawa akina dada inabidi hii kesi waivalie njuga. Ikibidi magazeti mengine na TV basi lifuatilieni hili.....

Ningelikuwa ni mimi, ningelifanya alichofanya Samuel L. Jackson kwenye ile film (samahani nimesahau jina). Ningelimsaka hadi nimpate hapohapo kwenye duka lake la kutengeneza simu na siku hiyo huyo Muhamed Kibaka angelikiona cha moto.

Hii ntakuwa naingia kuilaani kila siku kwa siku tano.
nimejisikia uchungu sana na kupandwa na gadhabu....dunia imekwisha walahi....

mkuu waandishi wako busy kuwahoji wanasiasa wanaowapa bahasha.....mamabo kama haya yanapewaha nafasi siku moja tu kisha yanakufa.....
 
Mwanakijiji na waandishi wengine,

Hawa POLISI na huyo kijana wanatakiwa WAISHIE KEKO. Kitendo cha kumaliza kesi kisirisiri inabidi kweli hii wachukuliwe hatua kali sanaa. Hawa akina dada inabidi hii kesi waivalie njuga. Ikibidi magazeti mengine na TV basi lifuatilieni hili.....

Ningelikuwa ni mimi, ningelifanya alichofanya Samuel L. Jackson kwenye ile film (samahani nimesahau jina). Ningelimsaka hadi nimpate hapohapo kwenye duka lake la kutengeneza simu na siku hiyo huyo Muhamed Kibaka angelikiona cha moto.

Hii ntakuwa naingia kuilaani kila siku kwa siku tano.
Inaitwa 'A Time to Kill'
 
Wakati nasikiliza kipindi nikajikuta kama hasira zimepitiliza kiwango cha kawaida...!
Ahhhh! Unaweza kujikuta unauwa mtu hivi hivi kwa hasira.
 
Yoyo, safi sana kwa kuleta ujumbe wako huu.

Ila hawa akina dada na kipindi kwa ujumla kama hakijakaa sawa vile? Na upuuzi wao wote wanaoutangaza (udaku like - kama hii ya tarehe 21/07/2009) wanatoa shule safi sana kwa kutumia lugha za mitaani zinazotumika mitaani. Kwa maana nyingine ni kuwa kipindi hiki kinakubalika sana mitaani kwani udaku huko unapendwa. Hongera akina dada kwa ubunifu, boss wenu na radio kwa ujumla.

Clouds FM mnafanya kazi nzuri saana. Keep it up.
 
Hii issue imeninyong'onyesha, kiasi nashindwa hata kuchangia mada zingine, nilikuwa nakula hata hamu ya chakula imenikimbia.
 
Hii ni zaidi ya unyama na ushetani. This guy must rot in jail and throw the keys.

Where is the law and justice.
 
Babu hii ni noma kabsaa, yaani hapo sheria haiitaji kusubiriwa ni kipigo tu mtaani...
 
Hakyanani, siamini kama jamaa yupo nje! whaaaat? hivi kuna sheria kweli nchi hii? si ajabu wakahitaji kufanya tena 'uchunguzi'!
 
Katika nchi nyingi zilizopiga hatua katika democracy na utawala wa sheria, vyombo vya habari vimekuwa katika nafasi muhimu katika kufichua uozo. Ninawapa pongezi sana Clouds, Ila lisiishie hapa kelele zipigwe mpaka wenye nyumba wasikie na haki kuchukua mkondo wake. Huu ni ubakaji na uharibifu, chukulia watoto waliharibiwa wangekuwa na wazazi polisi, si kesi ingekuwa imeisha?.

Mambo kama haya ndiyo yanaharibu nchi, kesho mtoto wa kigogo akimtemea mate traffic barabarani, itakuwaje?, atamwacha kisa mtoto wa kigogo?. Sheria ni msumeno. Huyu kijana mwalibifu na polisi wote waliohusika na kumwachachia huru wawajibishwe.
 
Dr. Slaa,

Heshima kwanza. Nafurahi upo hapa na hili jambo umeliona. Sintasema ufanye nini kwani itakuwa ni kukufundisha kazi ambayo siku zote unaifanya kwa uimara mkubwa. Labda niseme "Thanks in advance" kwa kulivalia njuga hili swala.

Jioni nzima ya leo nafikiria kama ingelikuwa huyo ni mtoto wangu na naona kila kitu kichwani kinazimika na ubongo kuacha kufanya kazi. Nafikiri unaweza kujikuta mtu unafanya jambo baya bila hata ya kujitambua.

Sijui future ya watoto hao itakuwaje. Ila ingelibidi viongozi waende kuwapa suport kwa walau kuwapa pole kwa yaliyowapata. Hapa sina maana ya kitendo cha kubakwa ila hiki kitendo kibaya kabisa cha POLISI kumkamata huyo kijana, kumuweka ndani na kesho yake kumuachia. Ndugu na jamaa wa mtoto lazima wajue JF tuko nao. Tutalipigia kelele hili swala hadi tuone mwisho na huyu kijana na POLISI waliomuachia, lazima wachukuliwe hatua kali.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwanza kabisa kwa masikitiko makubwa na moyo mzito (kumsikiliza huyo mtoto kumeniumiza sana) nataka kulaani ufirauni huu kwa maneno makali kabisa.

Pili ningependa zaidi kuona mchakato mzima wa ku expose mambo haya unafanywa bila kuwaondolea dignity na privacy waathirika.Kwa jinsi kipindi kizima kilivyoendeshwa kwa mtu anayeelewa privacy na dignity ni kama vile hawa watototo wamekuwa raped twice, kwanza na huyo baradhuli halafu tena hapo Clouds FM.

Sijui version yetu ya FCC iko wapi, na nini kinaweza kutangazwa hewani na nini hakiwezi.Hapo katika ku expose hii issue kuna mabaradhuli wengine wanapata ideas, kuna wengine wataiona kama Clouds FM walikuwa wanaifanya hii situation kuwa worse, kama kuna watu sadist waliokuwa wanapata satisfaction out of this, at least there can be argued to appear the possibility of this, which cannot be allowed, not even the appearance kwamba sadists watafurahia kufanya hii interview.

My point is, there has got to be a way to expose these ills with dignity and privacy.Sikuona hii Clouds FM. Hao watangazaji wenyewe wana come across kama hawa appreciate the depth and gravity of this situation. Hivi Tanzania hakuna mtoto siku hizi?

Sijui kama ndiyo mambo ya kibongo bongo yanavyokwenda lakini firstly it is very disheartening and secondarily it is rather dehumanizing, instead of helping the victim, the whole circus ends up raping the victim once again.There has got to be a better way.
 
Back
Top Bottom