clouds fm yatusaliti!
the whole week pj wa power breakfast (clouds fm) alikua anatembelea migodi ya barrick. Akaja na bla bla bla kwamba wamepeleka maendeleo katika vijiji vilivyo zunguka migodi. Mie nimemuona yeye na waliemtuma kwamba ni wa puuzi. Sababu ni hizi:
1. mikataba ya migodi ni mibovu
2. tunapata only 3% from revenue ya madini
3. migodi imetililisha sumu katika mito kama tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa
4. watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua.
leo hii pj na power breakfast, niseme cluods fm wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu?
pj, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Hao jamaa wanafanya pr ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo. Mimi na wewe pj tutabaki hapa hapa tz. Hiyo cheap pr unawapa haitafautiani na ile ya richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!
ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na liyumba je? Anashutumiwa kuiba tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi?
Sasa nikuulize pj, hao jamaa zako wa barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba bot tuka invest katika migodi yetu?
huu ni ujinga watu kama pj na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa.
ombi langu kwako pj na wana clouds wenzako nikwamba, watz waleo sio mbumbumbu. Tunaelewa. Tunachambua na tunatafari. Huwezi tupumbaza kamwe.
mjadala unaendelea.