Clouds lazima watambue kuwa hawana nguvu ya kufanya kila watakacho

Anayelipa matangazo ni vodacom na kampuni zingine, msanii halipi kutangaza chochote. Na vipindi vingi vinawahitaji kwa ajili ya interview hasa wasanii wakubwa

Sent from my SM-J320F using JamiiForums mobile app
 
Wote maboya tu ila kikubwa tuone nani mshindi kati ya clouds in general na ruge wao VS bashite na WCB yao.....sa HV aslay namuona anatengenezewa njia alafu huku bashite anatia baraka ya kufungua radio na TV za WCB
 

Mimi nimeshangaa sana Diamond na Managers wake kuingilia utoto na ujinga uliofanywa na Iyobo, kwanza wangetakiwa kumkanya na kumpa onyo kali siyo kuwa upande wake maana alichofanya ni ujinga, uhuni na jinai. Nimeshangaa sana jambo dogo linashupaliwa utadhani cjui nini kimetokea, kweli hii nchi wenye busara wameisha. HIZI TIMU UCHWARA ZITAWAANGAMIZA WASANII WETU, KWANINI HAWAJIFUNZI KWA VILABU VYA MPIRA AMBAKO CLUB IKO TAYARI KUMPA MCHEZAJI WAKE ADHABU HATA KAMA NI STAR KIASI GANI AKIFANYA UJINGA UJINGA.
 
Wote maboya tu ila kikubwa tuone nani mshindi kati ya clouds in general na ruge wao VS bashite na WCB yao.....sa HV aslay namuona anatengenezewa njia alafu huku bashite anatia baraka ya kufungua radio na TV za WCB
matapishi
 
hujuwe unachoongea
 
UFALME NA U-MUNGU MTU WA CLOUDS UNASIMIKWA NA WASANII WENYEWE.

Kwenye wimbo wa Bongo Hip Hop wa FidQ kuna mstari unasema hivi:-

"Sio tu BONGO mpaka NG'AMBO hakuna UHURU wa HABARI... kuna uhuru wa mwenye CHOMBO, MITAMBO na mwenye MALI... Kujifanya hawasikii, haiwasaidii, wala HAIWAJENGI... Unachosema ni kamwe IPP haitompinga Mengi."

Mstari huu unanifunza kwamba huu uhuru unaoliliwa sana na wasanii wetu ni ngumu sana kupatikana ama hata kuuona tu sababu dunia nzima uhuru upo kwa mwenye chombo, mitambo na mali na huu ndo ukweli ambao ni ngumu sana kuukubali.

Lakini kabla ya kuanza kuvilaumu hivi vyombo vya habari Serikali yetu kupitia sekta za sanaa wao wanamitazamo ipi juu ya hizi sanaa? Je haya malalamiko yanayotolewa na wasanii kila mara wao hayawafikii? Na kama yanawafikia huwa wanayaweka kwenye droo za meza zao tu (kupuuza)? Au bado wanayatafutia ufumbuzi? Lakini pia hizi taasisi (Wizara ya Habari, michezo na BASATA) zinaSERA zenye mwongozo wa kuielea sanaa ya Tanzania? Haya ni maswali ambayo miye binafsi najihuliza.

Tatizo lingine wasanii wetu wa Bongo chombo cha habari wanachokipa thamani na kukitumainia ni Clouds fm pekee, yaani ni bora redio zote zisipige wimbo/nyimbo yake/zake ila ukipigwa Clouds tu kwake ni faraja tosha. Nyimbo za Diamond EAST Africa Radio hawapigi ila sijawahi kusikia meneja wa Mond kutoka hadharani na kuwanyoshea vidole ya kwamba kwa nini hawapigi nyimbo za Mond, ila kutopigwa kwa Clouds tu wamekuja juu, hapa najifunza kuwa ufalme na huu tunaouita U-Mungu mtu wa Clouds unapandishwa na WASANII WENYEWE.

Clouds fm wapo vizuri kwenye suala zima la kutoa 'PROMO' kwa wasanii hivyo wanauwezo mzuri wa kumpandisha msanii na kumfanya hajulikane hilo ni ngumu sana kupingwa, sasa ukikubali kubebwa kinachofuata ukubali na kushushwa. Kwenye wimbo wa hawatuwezi wa Nako 2 Nako Lord Eyes anasema;

"Yule yule anayekupandisha ndo yule atakayekushusha"

Bahati mbaya au nzuri Mond Clouds walimbeba wakati anaanza lakini leo hii Mond anajibebesha ama kujibeba mwenyewe hivyo ni ngumu sana kumshusha sababu hujui amejibebeshaje mpaka kufika hapo halipo. Lakini kwenye wimbo huo huo wa hawatuwezi Lord Eyes anasema tena;

"Macho kwenye fedha dizaini ya mbwa msaka fedha... Huu sio mchezo ni vita na hivi ndo tunavyovicheza"

Kwenye huu mstari namuona DIAMOND kwa namna anavyozitazama fedha kwa jicho la uchu, kwa namna anavyoumiza akili kuzitoa pesa zilizo ndani ya kichwa chake na kuzileta kwenye uhalisia wa makaratasi wakati anayafikiria yote haya anatambua kuwa mafanikio yake hayaletwi kwa dhana rahisi ya uwanja wa buradani ila anaamini yupo kwenye uwanja wa vita ni lazima apambane vilivyo ili aweze kufanikiwa / kushinda.
 
hujuwe unachoongea

Inawezekana sijui ninachokisema ila ingekuwa vema ukanielewesha maana mimi naona bifu ambalo sijui linatoka wapi . Kabla sijachangia niliuliza nini sababu ya hayo yote kuna mdau akajibu ni sababu ya Iyobo na Shilawadu na ndiyo maana nikajibu hivyo hapo juu. Sasa naomba ndg unieleweshe nini hasa sababu ya yote haya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…