Clouds Media kuendesha shindano la DC bora, RC bora na Waziri bora. Washindi 5 wa kwanza kuzawadaiwa!

Kwani ni dhambi kumkosoa?
 
Mashindano yote lazima yawe na kibali kama wana vibali mimi ni nani nipinge?
 
Jana Magu alisema kuna ma DC/RC wanapenda kuonekana kwny ma tv ili waonekane wapo tu ila hakuna wanachokifanya.
 
hizo nafasi ni nyeti sana ila kwakuwa waliopewa wengi ni hawana uwezo, basi nafasi hizo zinaonekana kama za kawaida sana hadi kufikia kipindi cha redio kuanza kuwajadili...kweli kazi ipo!!!. Hizo nafasi zina hadhi yake kubwa sana ila wengi wa waliopewa dhamana ya kuzifanyia kazi wanapwaya......sasa inakuwa ni kituko. Alafu nchi ishakuwa na wasomi wajuaji wengi sana, hadi kudharau vitu vya msingi. Hivi wanashindanishwa watu au nafasi?😛
 
Ndio, ni dhambi kama hutumii njia rasmi. Kama una maoni, nenda kwenye Tovuti ya Ikulu au Idara ya Habari - Maelezo, yatoe hapo.
Mkuu rudia kusoma ulichoandika, kama hakijakuchekesha basi una tatizo la bandama.
 
Huu ni uchemfu wa Kiwango cha A+. Kweli clouds ni Ruge , na hivi anaumwa Basi akina Ngoma wanachemka. By the way waangalie wenzao TWAWEZA wanavyo nyolewa. Believe me hapa clouds wamebugi saaana
 
Huu ni mchanganyiko wa utoto, upumbavu na upuuzi wa hali juu. Uzwazwa wa populism kuna wakati unawafikisha watu hapo. Watanzania walivyo wajinga na malimbukeni, watashiriki kwenye hizo kura mshenzi. Watu badala ya kufikiria na kufanya maamuzi kwenye mambo ya maana kwa mustakabali wa maisha yao, wanahangaika na mambo ya kishamba. Kujipendekeza ni mzigo pia.
 
Wanafanya ujinga! Ila itakuja kuwatokea puani hata kama sio leo!
 
Nalipinga hili shindano, kuna viongozi bora kabisa na hawafanyi mambo kwa media na nina uhakika wanaweza hata wasifikiriwe kuwa wapo. Naapa pia waziri bora atakuwa adui wa Magufuli hadi 2025.
 
Vigezo vinavyotumika kumpata huyo kiongozi ni vipi au jinsi gani kiongozi husika amefanikisha wizi wa kura na kunyanyasa wapinzani?
Hata namna alivyofanikisha Fiesta 2018 ni kigezo pia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…