Clouds Media na Shafii Dauda: Gharama za Kufuatilia Michezo kila Kombe Duniani

Clouds Media na Shafii Dauda: Gharama za Kufuatilia Michezo kila Kombe Duniani

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
Kwanza nianze na kushukuru sana kwa kazi inayofanywa na Radio na TV ya Clouds ya kutuhabarisha matukio mbalimbali ya michezo duniani.

Nimeona Kazi ya Shafii Dauda kuwa ni nzuri sana. Amekuwa akifualitilia kwa undani sana matukio ya kimichezo katika mataifa mbalimbali. Nimeona ameenda Kombe la Dunia Brazil na akaleta matukio karibu yote. Pia ameenda Kongo kwenye Klabu Bingwa Afrika na sasa nimeona yuko Japani katika Kombe la Dunia la Klabu Bingwa.

Ila nimejaribu kufikiria, nani anagharimia safari hizi?

Najua ni ghali sana kuishi nje ya nchi pamoja na usafiri. Je ni Clouds media inatoa sapoti kwa Shafii? Na kwa nini si wengine kama Lwambano na sasa naouna Maestro kakimbia?

Lwambano nasikia kaenda Ethiopia na Uganda tu tena na timu ya Taifa.

Sina shida na hili ila nimeona niandike, ili makampuni mengine yaige kusaidia wafanyakazi wao.
 
IMHO, japo nina akili ndogo ila huwa nahisi nina akili kubwa kuliko hawa wachambuzi wa soka wa siku hizi.

Dr. Leakey ninadhani kanizidi akili.
 
Na mim huwa najiululiza swali kama lako kwamba anawezaje kusafiri namna hiyo?
 
Ukiacha Huyo pia Kuna Maulid Kitenge naye mda mwingi yupo nje ya Nchi sijui nani anamlipia?
 
Sijafuatilia sana Maulid Kitenge, ila Shafii hata kuwe mkutano wa namna gani FIFA au CAF huwa anaenda, achilia mbali makombe na kusafiri na timu nje ya Afrika. Maana nakumbuka hata timu ya watoto ile ya Alliance, Mwanza ilikwenda Ujerumani alienda nayo. Afrika Kusini na London kuna mikutano ya Michezo anaenda. Mwisho najiuliza Clouds Media inawezaje kumsapoti mtu mmoja tu kwa namna hiyo?
 
Dauda ana mkataba na startimes na Dstv so hao ndio wanamsafirisha mara kibao ndio maana kma unafatilia updates zake utaona either kaipaisha Dstv or Startimes
 
Lwambano Lugha Inampiga Chenga Kidogo, Kuna Siku Alikuja Mgeni Wa Kizungu Kwenye Kipindi Chao Cha Sports Bar Pale Clouds TV Hakika Lwambano Alipata Sana Shida na Bila Msaada Wa Shaffih Dauda Jahazi Lingezama Siku Ile lakini Hata Huyo Shaffih Nae Sio Kwamba Anajua sana Ila Jamaa Anajitahidi Sana Kujituma Huku Makampuni Makubwa Kama Star Times na Dstv Yakimsapoti.
 
Ngoja nijiweke kwenye nafasi ya kumiliki clouds media:

Ningepeleka Shafii Dauda kwa sababu moja tu. Quality ya kazi ile ninayotaka akaifanye. Ukiniuliza ina maana wengine wale hawana quality?! Jibu, hata kama wana quality lakini hawawezi kulingana, lazima awepo mmoja bora zaidi na huyo bora zaidi ndio nampeleka huko, after all huyo ni mchambuzi 'senior'!
 
Acha nichekeeee!!!!

Itakuwa nzuri ila angetumia mwanya kama huo kupata network kubwa zaidi hasa kuwa wakala wa wachezaji kwa nchi za Africa Mashariki.

Maana naona yeye na Simba tu na mpira wetu ndo huu.
Lwambano Lugha Inampiga Chenga Kidogo, Kuna Siku Alikuja Mgeni Wa Kizungu Kwenye Kipindi Chao Cha Sports Bar Pale Clouds TV Hakika Lwambano Alipata Sana Shida na Bila Msaada Wa Shaffih Dauda Jahazi Lingezama Siku Ile lakini Hata Huyo Shaffih Nae Sio Kwamba Anajua sana Ila Jamaa Anajitahidi Sana Kujituma Huku Makampuni Makubwa Kama Star Times na Dstv Yakimsapoti.
 
Alikuwa juu ya Maestro? Maana najua mtu kama Maestro na Kibonde ndo wanamichezo wakongwe pale pia alikuwepo jamaa alikuwa anaitwa Jimmy Kabwe.
Ngoja nijiweke kwenye nafasi ya kumiliki clouds media:

Ningepeleka Shafii Dauda kwa sababu moja tu. Quality ya kazi ile ninayotaka akaifanye. Ukiniuliza ina maana wengine wale hawana quality?! Jibu, hata kama wana quality lakini hawawezi kulingana, lazima awepo mmoja bora zaidi na huyo bora zaidi ndio nampeleka huko, after all huyo ni mchambuzi 'senior'!
 
Kuna mtu anadai kuwa sio mara zote Shafii Dauda anaposema yupo nje ya nchi basi ni kweli yupo nje ya Nchi, mara nyingine anakuwa hapa hapa Tanzania. Kuna kipindi alidai yupo nje ya nchi ila kumbe alikuwa amejichimbia Morogoro, katika kijiji kimoja cha huko Mahenge.

Mimi nilishindwa kumwamini huyo jamaa.
 
Sitaki kukubishia maana kuna wakati Millard Ayo alikua anasema anaripoti LIVE kutoka nje ya nchi LAKINI niligundua HAIKUA KWELI bkoz mitambo ilikorofisha sauti ya Ayo ikajirudia mara tatu mfululizo kusema neno hilohilo. Nilagundua WAMEREKODI sauti tu. The same kwa 'njia panda" walikua wanapandikiza sauti ya Dr. Isaac Maro kama sio mjanja utadhani yupo studio Mikocheni kumbe yupo Japan. Napenda watangazaji WASIODANGANYA wasikilizaji
 
Back
Top Bottom