Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Kwanza nianze na kushukuru sana kwa kazi inayofanywa na Radio na TV ya Clouds ya kutuhabarisha matukio mbalimbali ya michezo duniani.
Nimeona Kazi ya Shafii Dauda kuwa ni nzuri sana. Amekuwa akifualitilia kwa undani sana matukio ya kimichezo katika mataifa mbalimbali. Nimeona ameenda Kombe la Dunia Brazil na akaleta matukio karibu yote. Pia ameenda Kongo kwenye Klabu Bingwa Afrika na sasa nimeona yuko Japani katika Kombe la Dunia la Klabu Bingwa.
Ila nimejaribu kufikiria, nani anagharimia safari hizi?
Najua ni ghali sana kuishi nje ya nchi pamoja na usafiri. Je ni Clouds media inatoa sapoti kwa Shafii? Na kwa nini si wengine kama Lwambano na sasa naouna Maestro kakimbia?
Lwambano nasikia kaenda Ethiopia na Uganda tu tena na timu ya Taifa.
Sina shida na hili ila nimeona niandike, ili makampuni mengine yaige kusaidia wafanyakazi wao.