Clouds Media ni media ya kinafiki sana

Wivu tu unawasumbua... hao ni team mond ndo wanaweweseka. Kwa taarifa yako hiyo tour kailipia ndio maana unaona ina promo ya kutosha.
Hili jamvi sasa mnataka kuligeuza kama jukwaa la siasa! Kule jukwaa la siasa, ukiongea kitu, may be against mtu wa UKAWA, utaambiwa gamba... na halikadhalika kama utaongea kitu against mtu wa CCM au CCM wenyewe utaambiwa upo UKAWA! Haya ni mawazo potufu, ambao kwa wenye kufuatilia jukwaa la siasa, hawezi kuchelewa kugundua kule kumejaa watu na stress zao! Hayo, ndiyo unayoleta wewe! Yaani kwavile tu mleta mada ameleta hoja in favor of Diamond, tayari umesham-brand kwamba Team Mond!!! Maajabu sana haya... umetumia vigezo gani? Bila shaka kama angeongea in favor of Kiba, ungemuita Team Kiba! Hivi unaweza kutaja sababu za msingi kabisa zilizokufanya umnasibishe na Team Mond pamoja na kwamba mwenyewe ameshaweka wazi kwamba yeye hayupo kambi yoyote? Humu jamvini kuna uzi kwa ajili ya mashabiki wa Diamond. Hebu nenda kamtafute huyo mleta mada kama utamkuta kule!

Tujifunze kujenga hoja kwa hoja badala ya hoja kwa viroja! Mtu kukimbilia kusema ni Team Mond na kwamba wanaweweseka, ni kiroja kama sio viroja na ni dalili ya defensive mechanism ya kutarajia kupata uungaji mkono upande wa pili!
 
Hii promo ya Alikiba ni too much hadi inakera, huo wimbo wake mpya hadi nimeanza kuuchoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…