Clouds Tv shida ni nini?

Tengeneza Njia

Senior Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
121
Reaction score
205
Jamani ni mimi au na wenzangu mmeona hiki!

Mimi ni mdau mkubwa sana wa chaneli ya Clouds kwa muda mrefu sana, lakini naona siku na miaka inavyoenda ubora(si wa vipindi pekee) na hata muonekano wa baadhi ya vipindi vyao umedorora! Issue ni budget, kukosa creativity au ndo dalili za kukata tamaa?

Mfano, kile kipindi cha kina Kipanya cha jioni(kuna siku mara wanagombaniana Oreo za KFC na yule Harris), wageni waimbaji wanaimba nyuma ya kitambaa cheusi, yaani quality ya muonekano ni doro kwa kweli! Ni kheri tubaki tu kuwasikiliza sauti zao badala ya kuendelea kuona tunavyoviona.

Tukiwa tunalipia ving'amuzi kuangalia cheneli tunazozipenda, basi na media mjitahidi kutupa kitu kinacholingana na gharama za mteja anazolipia, plus muende na kasi ya kidigitali iliyopo!
 
Wasafi wamewapiga bao mkuu, wana tour kama ilivyokua fiesta. Wana mavipindi ya vijana wa masiku haya.

Clouds haieleweki ni channel ya siasa, michezo au burudani. Vipindi vyao hubadilika kulingana na upepo wa kisiasa wa wakati huo.

Wasafi wao wamebase kwenye michezo na burudani kama ilivyokua clouds ya late Ruge na ishu nyingine kwa mbaali ila kwa sasa siasa humo humo. Sifia sifia ya watangazaji wa clouds itakuacha kinywa wazi.

Ukiangalia kipindi cha msumari wa moto cha wasafi na kile cha kina kipanya clouds wale jamaa wanajockes za ajabu ajabu sana kazini.
 
Utaskia oktoboa septembeka sensabika jamuhuri ya tozo
 
Ni vumbi tu nalo litapita upepo ukitulia.
 
kwani mawingu yakipigwa na upepo si yanasambaa hayawi na uzito tena.
ndo clouds walivyopigwa na upepo wa wasafi alaf wakaja wakapigwa na upepo wa kuge kutata moto bas saa hzi wanapost hadi b/day ya mtt wa kusagwa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli kabisa hiko kipindi wanakiita sentro actually ubunifu wa kile kipindi ni mzuri sana na vile ualika wageni mbalimbali ila shida yao ni moja kuna mambo hufanya mbele ya kamera uwa siyapendi mfano

Iko siku wanaleta habari za ubishani juu ya familia zao kitu ambacho hakituusu

Ila pia vile muda mwingine yule mwongoza kipindi babra anavyokomandi mambo either kwa mtoa habari kuchelewa ni kama hawakujipanga lakini pia uonesha uso wa hasira wazi wazi

Kipindi ni kizuri ila wanaokiwasilisha wapunguze uswahili na wawe serious na kipindi tu
 
Bora usome nyuzi za wadau humu jf kuliko kuanza kusikiliza makelele ya watangazaji wa enzi hizi, angalau ITV kiasi watangazaji wanasikilizika.
Heeeh! ITV tena!!!??? Hiyo ndo TAKATAKA kabisa.
 
Nadhani hata watangazaji wenyewe wamebaki ki-maslai tu kwa sasa (mpunga si unaingia?) hayo mengine wanaona wawaachie BBC!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…