Cloutus Chama hana thamani hii

Usajili wowote ule ni kamali, hata kama mchezaji fulani kufeli kwenye klabu mpya hutokea kwa nadra sana, lakini itoshe tu kukubaliana kwamba huwa inatokea.

Ni kweli Chama sio BIMA kwa timu ambayo yupo kwamba isifungwe. Na hakuna mchezaji duniani ambaye uwepo wake kwenye timu yako unakuhakikishia kwamba hautafungwa.

Kuhusu bei, hilo ni suala la "negotiations" hakunaga bei elekezi za wachezaji.
Hiyo milioni 200 inaweza ikatosha, au ikawa kubwa sana au ndogo sana kulingana na namna mtakavyo negotiate mezani baina ya pande zote husika.

Mawakala hiyo ndio kazi yao, ni kazi halali, hata Ulaya akina Mino Raiola wanafanya hivyo hivyo. Inabidi tuzoee.
 
Nakuelewa nakuelewa unajua hata kwenye darasa la wajinga tupu kunakuwa na best student....
ndio Chama kwa soka la Tz
 
Hana thamani ipi? Maana mtoa mada hajataja hiyo thamani ila cha ajabu mwenzangu umemuelewa kama hutojali unaweza nisaidia namie mtoa mada anaongelea thamani ipi mkuu
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umri umemtupa, uwezo wa kucheza hana tena. Ndiyo maana waarabu hawamtaki tena.

Kwa lugha nyepesi tunasema ameishafeli maisha ya soka ingawa okotaokota watamchukua tu kwa sababu wanapenda kuchukua wazee.
Sizitaki mbichi hizi
 
Hapo kwenye bei ndipo madalali wanapohusika na manipulation ya vilabu. Timu mbili pinzani zinachombezwa ziingie kichwakichwa kwenye mkenge. Bei ya Peter Banda, Yusuf mhilu, yanick, Aucho zimepandishwa juu na walevi kwa kutumia ulevi wa walevi.
 
Kwahiyo unataka kusema Maguire (Halima Gwaya) aliyenunuliwa kwa mabilioni ya pesa anamzidi kiwango Mwamnyeto au Kennedy Juma waliosajiliwa kwa Milioni chini ya 100, kwakua yeye anacheza Manjesta? Wana Bissaka anamzidi kiwango Asukile ama Kapombe kisa Bissaka anacheza EPL na alinunuliwa 50M Paund?
 
Ewaaaa!! Huo ndio ukweli wenyewe. Ndio maana kila taifa la Africa linaita na kutumia wachezaji wake wanaocheza Ulaya wakati wa mashindano ya timu za taifa. Mbona Tanzania tunang'ang'ana na Mbwana Samatta kwenye kila mechi? Tena tumempa unahodha wa timu wa kudumu hata kama mchango wao sio kivileee.
 
Experience matter.
 
Sizitaki mbichi hizi
Timu za Ulaya zina jicho la mwewe, hawazi kuacha kumuona mchezaji mzuri na kumpeleka kwao. Tena Zambia Kuna mawakala kibao kabisa, kwanini jicho la mwewe halikumuona Chama? Chama Hana tofauti kubwa na akina obrey Chirwa, Rally Bwalya, chikwende, nitamshangaa mtu akitoa 6m kuleta Chama kwenye timu. Hana thamani hiyo bhana!!
 
Wamisri hawamuelewi anaruka ruka tuu uwanjani, wanamuuliza kocha masmane kasajili ka emoro cha nini na kwanini anakapanga kamtu kalikoshindwa kwenda sambamba na michezo ya watu walioshiba wenye mchezo wa kasi wanataka kumtoa roho
Ila jamaa ana msimamo sana aliwawashia moto balaa.......naona tau ndio balaa pale alahly
 
ndio maana alipo sasa ni failure tu
 
Heh we ni mwanamichezo kwel

Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
 
Hana thamani ipi? Maana mtoa mada hajataja hiyo thamani ila cha ajabu mwenzangu umemuelewa kama hutojali unaweza nisaidia namie mtoa mada anaongelea thamani ipi mkuu
Umeamini sasa kuwa hana thamani aliyoondoka nayo? tumepigwa kiboya. Karejeshwa kisa anatajwa kusajiliwa na Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…