Cloutus Chota Chama na Mo Dewji mambo safi

Kwani nimebisha mkuu,nakuunga mkono 100% alichofanya Mo kwa Chama sio kitu kizuri,ila kwa sasa Mo na Chama wameonyesha kusameheana,shida inakuja,je'kwa wale waliomkunjia Mo kwa kitendo chake cha kumdis Chama na wao watakunjua nafsi au bado watabaki na chuki zao kwa Mo?
 
Bado haibadili chochote kuwa muhamedi ana mambo ya kitoto.
 

Hatuna chuki, tunalinda heshima ya taasisi ya simba. Tusipokemea haya itafika mahali kutakuwa na wachezaji wa mo na wachezaji wa simba na baadae kutakuwa na timu mbili ya mo na simba kama ilivyo yanga na pan Africa. Kiungwana mo anatakiwa kuiomba radhi simba yaishe
 
Chama ameonesha hekima kubwa na kuwa yeye ni professional siyo tu kwenye mpira, bali hata kichwani yupo vizuri.
Mo ni mkubwa kwa Chama, lakini chama amesha ukomavu mkubwa kupitia kauli yake.

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
Hongera Chama; hongera Mo. Huo ndio uanaume sasa kumaliza mambo kiutu uzima. Kwenye maisha kunakupishana kauli halafu baadaye mnakuja kuweka mambo sawa kwani maisha yanaendelea. Naamini Mo amepata somo zuri na hatorudia kosa la kiufundi alilolifanya kwenye ukurasa wa Insta wa Chama.
 
Wana uto hawajui kitu kimoja mo ni shabiki na mwanachama kabla ya kuongeza na udhamini juu jiulize mtu wa aina hii hajajibu kashifa afu kuna mtu anatoa sifa kiuhalisia wote wanapaswa kujihoji
 
Mo sijui ni umri au ana utoto wa mama kudekezwa anapoishi nyumbani kwao,mbona matajiri wengine maarufu wa Bongo atuwaoni wakidemka mitandaoni kama huyu Mo?
 
Manara ndio anafanya Boss wenu awe mswahili?

Kwani tokea lini MO akawa sio Mswahili? Kama unajua nini maana ya Mswahili basi MO ni mswahili pure. Upumbavu wa Watanzania ndiyo unawafanya muone kuwa Mswahili maana yake ni Mjinga.
 
Kwani tokea lini MO akawa sio Mswahili? Kama unajua nini maana ya Mswahili basi MO ni mswahili pure. Upumbavu wa Watanzania ndiyo unawafanya muone kuwa Mswahili maana yake ni Mjinga.
Tabia za kimaskini hizo.

You cant see.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…