Club House na Space ndiyo vijiwe vya sasa hivi

Club House na Space ndiyo vijiwe vya sasa hivi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Club House na Space ni social media rooms zinazoruhusu majadiliiano ya wazi. Hivi karibuni zimetumika sana na wana siasa kuongelea hali ya siasa za Tanzania. Faida mojawapo ya social media ni kuunganisha watu walio sehemu mabali mbali za dunia.

Kuna kijana graduate nilikutana nae, aliniambia ameshaacha kutembeza CV kwa sasa. Baada ya kuhangaika sana aliamua kukopa hela na kununua wheel barrow, smart phone na speaker ndogo ya iPhone alipewa na rafiki yake kama zawadi.

Anakwenda mahakama ya ndizi asubuhi na kununua machungwa, ndizi, maembe, pears zabibu (kutokana na msimu) na kuweka kwenye wheel barrow yake. Mchana walio kazini wengi hununua matunda lakini jioni club house na space vikianza, vijana humzunguka na yeye anaunganisha spamart phone na speaker na wote wana sikiliza.

Siku za Club House na Space wasikilizaji humuunga kwenye biashara na huweza kumaliza matunda yote. Akishatoa mtaji anapata 30,000-25,000 faida. Kwa sasa anakata 10,000 kwa siku kulipia wheel barrow.

Mtaji wa masikini ni nguvu zake.
 
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa, sema sasa uzito unakuja pale kutembeza matunda wakati una 4.2 GPA na ulikua unapokea 7500 kila siku kutoka bodi.
Uzito wako utakulaza njaa na kukukosesha mademu na kukuletea ulemavu kisa kupiga P.
 
Kama kuna mtu ana muunga mkono kijana graduate kutembea na radio. Na eti mtoa thread nae kaonekana ametoa story of thought. A touching story kama kuna anayemuunga mkono. Haya aendelee. Ila mimi nasema huyo dogo ni MPUUZI. Tena saaana. Yaani aweze kuuzia matunda huko club house. Ashindwe kabisa kufikiria jambo la shughuli kama msomi.
 
Sijaona uhusiano wowote wa kuuza hayo matunda na masuala ya Space na Clubhouse....

Alafu Space nyingi hazihusu siasa asilimia kubwa ya Soace zinahusu masuala ya Technology hasa Web 3 na Online earning.
 
Back
Top Bottom