Muungano wa Asasi Za Kiraia unaotetea Haki ya Upatikanaji wa Taarifa (Coalition on Right to Information - CoRI) umelaani vikali uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuisimamisha kwa siku 90 JamiiForums, jukwaa maarufu la majadiliano na uwazi nchini Tanzania.
Uamuzi huo umetangazwa Septemba 6, 2025, na kulingana na barua ya TCRA kwa Vapper Tech Limited (JamiiForums), ulitokana na madai ya kukiuka masharti ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni) za mwaka 2020, zikiwemo kuchapisha taarifa “zisizo sahihi na zenye upande mmoja” kwenye tovuti na akaunti zake za mitandao ya kijamii, pamoja na kushindwa kudhibiti maudhui yasiyofaa dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo, CoRI imesema kuwa hatua hiyo ni kinyume cha Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, hususan Ibara ya 18 inayotoa haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa. Pia imetajwa kuwa inakiuka mikataba ya kimataifa ikiwemo Mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), Kifungu cha 19, na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, Kifungu cha 9, vinavyolinda uhuru wa maoni na upatikanaji wa habari.
“Kusimamishwa kwa JamiiForums sio tu kunadhoofisha haki za kikatiba bali pia kunahatarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na mijadala ya wazi ambayo ni nguzo za demokrasia,” amesema Mwenyekiti wa CoRI, Ernest S. Sungura, katika taarifa hiyo
Muungano huo pia umepinga jinsi mchakato ulivyofanywa, ukieleza kuwa JamiiForums ilitakiwa kujibu tuhuma hizo siku hiyo hiyo, bila muda wa kutosha kuandaa utetezi
Kwa mujibu wa CoRI, “kusimamisha JamiiForums hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi kunawanyima wananchi mamilioni wa watumiaji wake fursa ya kupata taarifa za kuaminika ambazo ni msingi wa maamuzi sahihi.”
Muungano huo umetoa wito kwa TCRA kuondoa mara moja adhabu hiyo na kurejesha upatikanaji wa JamiiForums. Pia umeitaka Serikali kuhakikisha kuwa hatua zozote dhidi ya vyombo vya habari na majukwaa ya mtandaoni zinazingatia misingi ya kisheria, uwiano na ulazima
“Tunatoa wito kwa wadau wote- wanahabari, wanasiasa, asasi za kiraia na wananchi kuendelea kutetea haki za msingi za uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa habari
Chanzo: Jambo TV