Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
Full Time: Simba inapata ushindi na kufikisha pointi 40 katika Ligi Kuu Bara.
Dakika ya 90, Meddie Kagere anaifungia Simba bao la pili kwa shuti kali.
Simba wanaongeza presha zikiwa zimesalia dakika saba.
Coastal baada ya kuwapa presha Simba wanafanikiwa kusawazisha bao.
Kipindi cha pili kinaendelea
Timu zote zinashambuliana kwa zamu, Coastal hawajataka kubaki nyuma kulinda, wanapanda na kuwapa upinani Simba.
Kipindi cha Pili kimeanza matokeo bado ni 1-0.
Kipindi cha kwanza kimekamilika, Simba wanaongoza bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison baada ya beki wa Coastal Union kujichanganya.
Mchezo ni mguu na timu zote zinashambuliana kwa zamu, ukuta wa Coastal unakuwa mgumu na Simba wanashindwa kuupita.
===================
Katika NBC Premier League, leo Ikiwa ni Karume Day, kuna mechi baina ya Simba Sc dhidi ya Coastal Union FC.
Simba wanataka alama tatu ili waendelee kujikita kwenye Nafasi ya Pili mwa msimamo wakati Coastal Union nao wanazitaka alama tatu ili wapande Ili wasiteremke Ligi Kuu.
Mechi hi itapigwa katika dimba la Uwanja Wa Mkwakwani, Tanga kuanzia saa 10:00 Jioni
Je, ni Mnyama ama Wagosi wakaya nani kuondoka na alama tatu?
Wagosi Wakaya Kunani Pale.
Scars
View attachment 2179085