Coco Beach pesa ya maegesho inaenda wapi?

Coco Beach pesa ya maegesho inaenda wapi?

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Ukifika Coco beach na gari utakaribishwa na mdau anayekusanya ushuru wa TZS 1,000 Kwa kila gari. Je, hiyo pesa inafanya kazi gani? Maana hata kile choo pale unalipia tena pesa. Uchafu umejaa kila kona.

NB: Halmashauri ya Manispaa waliwahi kupewa maelekezo ya kuendeleza usafi hapo Coco Beach naona wamenogewa asali, wanabunya tu.

EiqrXKWWAAEEIHw.jpg


PMO_7741.JPG
101975992_3185450501521972_3966665901473792000_n-1024x1024.jpg
 
Wewe lipa tu Mkuu, kama ushuru unakusanywa maana yake unaenda Mamlaka husika, halmashauri ni mawakala tu. Wakishakusanya pesa wanasubiri gawio si kujipangia matumizi ya mapato.
 
unashangaa pesa ya maegesho coco beach. Yani hapo kariakoo unajenga gorofa lako na kuwepa parking ya wateja unashangaa kuna mtu anakuja kusimamia ushuru wa maegesho utazani kwake
Hii kitu inashangaza sana, mtu kajenga jengo lake la kibiashara pale mbele ni eneo lake na analenga wateja wenye magari waegeshe magari ili waingie kupata huduma, halafu anatokea mtu wa jiji anaokota parking fee kwenye eneo ambalo siyo mali yake na hajawekeza chochote.

Haya tuseme wanazuia mlundikano wa magari katikati ya jiji, vipi huku mitaani hizi parking fee hadi kwenye maeneo ya strarehe kama kwenye baa wanachukua kwa lengo gani hasa........au ndo pesa zinatafutwa kwa udi na uvumba kulipa madeni.​
 
Hicho choo cha Coco Beach ni kichafu balaa sijui kwanini wanazuia watu wengine wasijenge,halafu kuna Dada linakaa hapo kukusanya Ushuru linajiona Sista Duu Balaa wakati ni libaya kama mimi na zaidi limezungungwa na harufu za Mavi.

Usiombe maji yakatike hapo ukifika chooni hakufai kwa harufu ya mavi na unaambiwa ukachote maji mwenyewe kwenye tank, hizo ndoo sasa ni chafu hazifai kama ni mtanashati au mrembo mapaparazi wakipata picha umebeba hiyo ndoo wanauzia kabisa Magazeti.

Ila hela anapokea tena kwa nyodo huku kajipiga mapoda.

Tanzania Wonders shall never end.
 
Back
Top Bottom