Cocochanel live interview on DJ sepetu show!!

Cocochanel live interview on DJ sepetu show!!

Mimi uwa sifikirii kama nina maadui, bali nawachukulia kama watu wanaopenda kunichakachua kivyovyote na hii inanipa motisha zaidi kubetter myself. Nawaona kama fans wangu

Siku zote naamini maadui siku zote ni watu walio nyuma yako kwenye mambo tofauti kama kukuonea wivu kwenye lolote maishani mwako ambacho hawana kama wewe.

Nikitoweka watanimisi kwasababu hawatakuwa na mtu wa kuwapa challenge wao kujiongeza. Na pia watayakumbuka mazuri yangu na nilivyowakimbiza na kuyaongelea.
Hahaha!
10.ni mtihani gani mgumu umewahi upitia maishani ila ukaja kugeuka kuwa jambo la thamani na unalojivunia!
Legacy yako,unataka iweje yaani alama zipi utaacha duniani kuonesha vizazi,cocochanel alikuwepo?
 
Furaha na Amani kwa familia niliyozaliwa nikijumuisha na wanangu kwa juuuuuuuu.

Pia mengine machache kwenye maisha kama nimeapia au nimeingia kwa kuaminia niliyovutiwa nayo juu ya kilichopo itabidi.. kutokana na yalivyo

Ninachokiaminia na kuamini kipo.. hata uniletee nini nitalishikiria.. na pia mtu akiwa mbishi au anaongea nami basi tu juu ya jambo bila kuwa na facts zilizoenda shule au proof ya kweli.. huyo nitakula nae sahani moja..
Nasukumwa pia maishani na machale niliyobarikiwa na Mola na hayaniangushi.

I hope nimekujibu.
Hivi ni mimi tu ama?
Simuelewi anachoandika kwa kweli

|No hard feelings|
 
Mimi zangu ni sijibu au sitendi kitu hapo hapo kutafuta chochote kama kumfurahisha mtu.. nitatafuta muda wangu wa kufikiria, kuchunguza inapobidi, yaani kupata nafasi inayobidi kujua iweje.

Pia kwangu ninakuja na kwamba ni msiri sana sana.. hata kitu kitokee siwezi kujiropokea kisa nimesukumwa kukasirika.. nitajiweka hata mtu usifahamu hilo limenijia.. naweza kukuchekea kama utaniona mjinga shauri yako.. so hapa inanipa muda tena kutotoa hata nilijualo hadi nipige pozi.. ukinipiga marungu pia utakuwa unajisumbua kama sitaki kuonyesha nimekasirishwa hadi nitafakari.

Naamini kujibu lolote hapo hapo mtu unaweza kujutia.. nitajibu huku niiangalie mbele pia na sio muda huo tu.

Samahani hasi na chanya maneno hayo naomba unifafanulie.

Seriously??
 
Hahaha!
10.ni mtihani gani mgumu umewahi upitia maishani ila ukaja kugeuka kuwa jambo la thamani na unalojivunia!
Legacy yako,unataka iweje yaani alama zipi utaacha duniani kuonesha vizazi,cocochanel alikuwepo?

Mimi kuna kipindi wazazi walikuwa nje ya nchi nasi kwa miaka michache. na hivyo ilikuwa ngumu sana walipotaka tusome shule za Tanzania.. nikaenda kusoma boarding school niliona kama nitashindwa kumudu na pia kwa kuishi nao mbali.. ila kwa kweli nilipokua niliwaelewa sana pamoja na kuwa na pesa za kutusomesha nje huko au nje ya ulaya n.k. hii kitu siijutii leo hii hasa baada ya kuja kusoma nchi za ulaya baadae.
Ilinifundisha mengi ya maisha na hivyo tangu sekondari hadi leo nikiwa nyumbani kwa wazazi ni kuwatembelea tu tangu warudi nchini miaka sasa.
Unajua ile ya kuwa independent woman basi hiyo najiona nimo
 
Napenda kumshukuru Mola kwa malezi niliyopewa katika kufundishwa mengi pia ya maishani na kuaminiwa na wazazi kuwa akili tulibarikiwa wote.. ni furaha sana kwangu.
Hii kitu nataka sana niipitishe kwa wanangu na kuhakikisha wao na cousins wao nao wanakuja kuacha mengi mazuri.
Hapa mfano mmoja ni sisi kuwa na marafiki wa kifamilia na kuheshimiana nao hadi leo hii kuishi vizuri katika shida na raha.. na wengine kwenye jamii na kutokuwa na maringo yotote ukibarikiwa au lolote kuishi vizuri na watu ambao huwezi kuona tofauti yangu kwao labda ujue. Na kuwaachia ya kuweza kujimudu mwenyewe kimaisha na kutokuwa mvivu na kujiamini kuanzia kwenye masomo, kikazi, kutokuwa na tamaa, kujali kujijengea jina kikazi na kibiashara bila kupitia mikato isiyo na maana na yakukushusha.

Bila kusahau kushindana na wanaume kwenye masomo kutafuta maksi za juu.. ha ha haaaaa niliwapa umiza vichwa.. kujiamini na kutokuogopa mtu huku ukiwa na heshima pia.
 
Mimi kuna kipindi wazazi walikuwa nje ya nchi nasi kwa miaka michache. na hivyo ilikuwa ngumu sana walipotaka tusome shule za Tanzania.. nikaenda kusoma boarding school niliona kama nitashindwa kumudu na pia kwa kuishi nao mbali.. ila kwa kweli nilipokua niliwaelewa sana pamoja na kuwa na pesa za kutusomesha nje huko au nje ya ulaya n.k. hii kitu siijutii leo hii hasa baada ya kuja kusoma nchi za ulaya baadae.
Ilinifundisha mengi ya maisha na hivyo tangu sekondari hadi leo nikiwa nyumbani kwa wazazi ni kuwatembelea tu tangu warudi nchini miaka sasa.
Unajua ile ya kuwa independent woman basi hiyo najiona nimo
Asante karibu kujibu maswali ya audience
 
Kwanza nj lazima kuweza kuongea na mtu kujua yupoje.. na hapo ndio ngoma inachezwa.
Awe na haya pia ujuzi wa mawasiliano, kusuruhisha matatizo kati ya wengine na lolote, awe msikilizaji, ajue kufanya kazi na wengine na kujishughulisha pamoja nao, awe anaaminika, na heshima n.k mengine machale yangu uingia pia na kumsoma mtu lugha ya mwili.

Haya pia ni muhimu kwa mtu ambaye yupo chini ya uongozi kuwa nayo.. na kuwa na ujuzi usaidia wa mengi ambayo wengi wanadharau.

Kama mtu amefaulu akaja kwangu kwa kazi, na hajawahi kufanya hata kazi ya kusaidia yoyote.. na aje mtu amefaulu chini yake yeye na labda alikuwa anauza vitumbua au maandazi mimi huyu ataweza kunivutia zaidi kumuajiri.. ni mengi naishia hapo.

Naona interviewee anazd kujidhihirisha kuwa yeye ni lemutuz
 
Back
Top Bottom