So, je uko salama, je dawa ya meno unayotumia haina kiambata hiki kinachosababisha cancer. By the way, Colgate walifanya utafiti miaka kumi ku-develop hiyo ingredient, na wakaiingiza kwenye dawa ya meno ambazo zilikuwa marketed kwenye zaidi ya nchi 100 kabla ya kuomba kukubaliwa kuingiza kiambata hicho kwenye dawa za meno zinazouzwa Marekani. Lakini, kwenye story pia kunaonekana udhaifu wa FDA ya Marekani ambayo inategemea ushahidi wa kisayansi wa kampuni za kibiashara kujua iwapo ingredient zina madhara kwa binadamu ama vinginevyo.
Kwa mujibu wa repoti ya Bloomberg, Colgate Total inayotengenezwa na kemikali moja inayojulikana kama triclosan inadaiwa kuongeza cells za kansa mwilini. Mamlaka ya kudhibiti vyakula na Madawa Tanzania (TFDA) imesema inafahamu kuwepo kwa hiyo ripoti na tayari imeshaagiza wataalamu wake kuifanyia kazi kabla ya kujua hatma ya dawa hiyo ya meno.
TFDA imeongeza kuwa Colgate Total imekubaliwa kutumika nchini baada ya mamlaka hiyo kuifanyia majaribio na kukuta kuwa ina kiasi cha asilimia 0.3 za triclosan ambazo hazina madhara ya kiafya kwa binadamu. TFDA imeongeza kuwa kiwango hicho cha asilimia 0.3 za triclosan kwenye Colgate Total zinafaa kwa matumizi ya binadamu wenye umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea.
Kwa mujibu wa The Citizen, Colgate Total inauzwa katika supermarkets na maduka mbalimbali nchini. Colgate Palmolive ambao ni watengenezaji wa colgate hapa nchini wamesema kuwa Total Colgate haina madhara kiafya, huku waki-cite mchakato wa FDA ya Marekani iliyofanya kabla ya kuidhinisha Total Colgate mwaka 1997.
Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti ya Bloomberg, mchakato wa maombi ya kuidhinishwa kwa dawa hiyo unaonyesha kuwa matokeo ya tafiti za kisayansi yaliyotumika kuonyesha usalama wa triclosan kwenye dawa hiyo hayakuwa ya moja kwa moja. Pia matokeo ya tafiti hizo yamewekwa hadharani mwaka huu pamoja na kuwa tafiti zilifanyika miaka kibao iliyopita.
FDA ya Marekani iliidhinisha dawa hiyo kutumia tafiti zilizodhaminiwa na kampuni inayomiliki dawa hiyo. Maombi ya kuidhinisha dawa hiyo yalikuwa na kurasa 35 zikijumuisha tafiti za ki-toxicology juu ya triclosan. FDA imeweka mchakato huo wa maombi kwenye tovuti yake kutokana na kesi iliyofunguliwa over a Freedom of Information Act request. Bloomberg News ilipofanya follow-up, FDA wakaamua kuweka mambo yote hadharani.