Combine harvester- kubota dc 60,dc 70

ipyax

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
4,247
Reaction score
6,578
Nahitaji combine harvester kwa ajili ya kuvunia mpunga ya aina niliyo itaja hapo juu.Nime ulizia hapa bongo bei yake ni kati ya milioni 75-85 kupitia kwa agent wao na sellers wengine wa mashine za kilimo.Pia nime ona za kichina kwenye mtandao ambazo zina fanana na hizo kwa design,size na muonekano lakini hazipo reliable na pia zina tabia ya kupoteza mpunga mwingi shambani wakti wa mavuno.Budget yangu ni kati ya 50-60 milion,kama mtu una idea itakayo niwezesha kuagiza hiyo mashine toka nje au hata kuipata hapa Tanzania kwa bei nafuu nita shukuru sana.
Mungu awabariki sana.
 

Kuna jamaa mmoja aliagiza yake kwa 30mil mpaka anaitoa, ni ya kichina inaitwa LIULIN labda uzi-google
 
Kwa bajeti uliyonayo kupata mashine nzuri ni ngumu sana. Ninafanya biashara hiyo ya kununua mashine za kilimo na kujengea barabara hapa UK na kuzileta Tanzania. Kwa msaada zaidi ni PM
 
Asante kwa usahuri wako kaka,nime ziona na zipo cheap lakini tatizo ni reliability yake pia na upatikanaji wa spea ni ishu.Hata zikiwa kazini zina tabia ya kupoteza mpunga wakati wa uvunaji.
Kuna jamaa mmoja aliagiza yake kwa 30mil mpaka anaitoa, ni ya kichina inaitwa LIULIN labda uzi-google
 
Asante kwa usahuri wako kaka,nime ziona na zipo cheap lakini tatizo ni reliability yake pia na upatikanaji wa spea ni ishu.Hata zikiwa kazini zina tabia ya kupoteza mpunga wakati wa uvunaji.
LIULIN hazipotezi mpunga kaka, ila tu container lake ni dogo hivyo mpunga kidogo tu ishajaa, so utatakiwa kwenda ku-offload mara kwa mara ambayo ni wastage of time.

Kuna jamaa alikua akiuza la kwake humu cheki na hii labda https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/913023-combine-harvester-mf-87-a.html
 
Hiyo ya jamaa nimeiona haoa jamiiforums lakini sio kwa ajili ya mpunga na pia ni ya matairi.Mpunga ule wa kwanza shambani kunakua na maji mengi kutumia combine ya matairi ni mziki,inayotumia chain ni bora zaidi.Kuhusu LIULIN nta check google nione bei zake zikoje na kama nina maswali zaidi nta kuuliza.Shukrani sana

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…