Combine ya Yanga ya Nabi na Barcelona ya Gadiora

Combine ya Yanga ya Nabi na Barcelona ya Gadiora

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Tuanze na first eleven za timu zote mbili.

Barca;
Kipa - Valdes.
Mabeki - Abidal, Mascherano, Pique, Alves.
Viungo - Bosquet, Iniesta, Xavi.
Washambuliaji - Pedro, Villa, Messi.

Upande wa Yanga;
Kipa - Diara.
Mabeki - Kibwana, Lomalisa, Job, Bangala.
Viungo - Sure boy, Aucho, Feisal.
Washambuliaji - Morrison, Mayele, Jesus.

Combine ni kama ifuatavyo;
Kipa: Diarra, kwa kusema kweli Valdes ni moja ya makipa wa kawaida sana waliopata bahati ya kucheza timu nzuri, sioni chochote anachomzidi mdaka mishale.

Right na left full backs: Dan Alves na Lomalisa hiyo haina ubishi.

Mabeki wa kati: Naenda na Job na Bangala, kwa mtazamo wangu Pique na Mascherano hawakua na ukali wowote, walibahatika tu kuwa kwenye timu inayomiliki mpira muda mwingi kwahiyo hawakua 'exposed' mara kwa mara.

Kwenye 'holding midfielder' ni pagumu sana kumchagua mmoja kati ya Bosquet na Aucho, ila acha twende na Bosquet kuhusu Xavi na Iniesta hao namba zao hazigusiki.

Pale mbele kwenye 'front three' Yanga bado kuna shida ya washambuliaji wa pembeni, ngoja kulia tumweke Messi na kushoto tumweke David Villa pale 'central staiker' ukizingatia Barca alikuwa anaanza na 'false 9' naona kabisa Mayele akidumisha namba yake.

Combine itakua kama ifuatavyo;
Kipa - Diarra.
Mabeki - Alves, Bangala, Job, Lomalisa.
Viungo - Bosquet, Xavi, Iniesta.
Washambuliaji - Messi, David Villa, Mayele.
 
Back
Top Bottom