Comedian na activist Eric Omondi ameachiliwa kwa personal bond ya KSh100,000 baada ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kudaiwa kuzuia magari kupita Kimathi Street, Nairobi. Eric alikanusha mashtaka hayo, akisema hana hatia. Kulingana na hati ya mashtaka, anadaiwa kushusha jerricans 120 tupu kutoka kwa lori, hatua ambayo ilisemekana kuathiri mtiririko wa magari jijini.
Mawakili wake, Danstan Omari na Babu Owino, waliambia mahakama kuwa jerricans hizo zilikuwa zimekusudiwa kusaidia wananchi kuhifadhi na kuchota maji. Pia walikosoa namna Eric alivyokamatwa katika uwanja wa ndege wa JKIA wakisema ilikiuka heshima yake.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa Eric alipuuzilia mbali wito wa polisi kabla ya kukamatwa. Kesi hiyo itatajwa tena Julai 2026.
Je, unaona Eric Omondi alikuwa akihudumia wananchi au alivuka mipaka ya sheria?
Source : Citizen Digital