Comedian Samuel Asubiojo asema Comedy inalipa kuliko udaktari

Comedian Samuel Asubiojo asema Comedy inalipa kuliko udaktari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Comedian wa Nigeria Samuel Asubiojo, ambaye ni daktari kwa taaluma amesema Comedy inalipa kuliko udaktari.

Asubiojo ambaye ni maarufu kama Mama Ojo alisomea udaktari wa binaadamu nchini Ukraine mwaka 2012 hadi 2018 lakini hakuwahi kupractice taaluma hiyo tangu hapo.

Kwa sasa anapata hela kwa kupitia video zake za vichekesho anavyotengeneza.

Je, hali ikoje kwa Tanzania, comedy inalipa kuliko taaluma?

1656063702351.jpeg

Picha: Samuel Asubiojo
 
Kama hakuna kazi na wasomi wakutosha hadi shoeshiner mtaani ana degree ya uhandisi hapo kinachofuata ni kujiongeza ilimradi ule!.
 
Labda comedy na uchawi wa Nigeria...

Dulivan mtoto wa juzi tu ila kipato chake kinawazidi ma daktari wengi tu bongo. Na dullvan hajazidi 27. Na hata kwenye game ya comedy hana miaka mitano
 
Maisha ya kina mpoki,jotti,masanja yakoje

Ova
 
Ni kawaida siku zote huwa kipaji kinalipa kuliko fani watu wanaoongoza kupiga pesa ni Hawa wanamichezo basketball & football musician kawaida sana
 
Basi watu wote wafanye comedy waachane na Taaluma hapo mambo ndiyo yatanoga, Kila mmoja atakuwa tajiri.
 
Kulipa ni nini ?

Tatizo kama binadamu tumepoteza muelekeo tunafanya kile ambacho mtu hupendi kufanya.., Mfano kazi ya ualimu inalipa kuliko ule ujira unaopewa (kwa mwalimu kuona mtu aliyemfundisha na amefanikiwa ni priceless)

Daktari sidhani kama ulienda pale ili upate fedha nyingi bali una moyo wa kusaidia na ukifanya hivyo ni priceless

Udaktari naweza kusema ni skill, tofauti na kipaji cha being a comedian huenda hata ukipewa skill usiwe the top comedian hence usipate hata senti na ukaambulia kuzomewa (hence anything done correctly na right marketing itakupatia pesa) comedian unaweza ukatoa kazi moja ukai-multiply kwa watu wengi ila ukiwa daktari huenda ikawa ngumu kufanya diagnosis kwa kutumia bluetooth au wi-fi

All in all to each his/her own....
 
Back
Top Bottom