Safi majibu mazuri, Swali je huyu mtu anaelewa chochote kuhusu uongozi wa taifa? ana elimu ya uraia? Namuunga mkono Ndugu yangu sikonge kwamba kabandika pale ile picha kama pambo tu ili na yeye aonekane anaenda na wakati. sasa kumbukeni 80% ya watanzania bara ndiyo wanaishi maisha yanayofanana na haya.
Bila ukombozi wa kweli tutaishia kusindikiza kikundi kidogo cha watu wanaojifanya ndiyo wanaweza kuongoza nchi hii. Bila kumshirikisha mtu huyu kiuchumi atajikwamuaje? tumwanche azame na kizazi chake? hamuoni kufanya hivyo si haki? kwani mali asili za taifa hili zinamhusu pia anatakiwa apate percentage yake.
Uzuri hajui haki zake kama mtanzania, anafurahia maisha yake na picha ya mgombea akiiangalia ni kama kafika beach hotel vile. Sasa kiongozi bora ni yule atakayeshirikisha watu wate kwenye nguvu za kiuchumi wa taifa letu. Mtu huyu na kizazi chake bila kumshika mkono nduguzangu kaishia huko huko porini kuishi kama mnyama.
Hana elimu, Hana afya, ni mgonjwa hana matumaini - Tunahitaji mabadiliko, tunajitahi kutoa matumaini mapya kwa watu wa namna hii waliokata tamaa kama huyu bwana tena kwenye nchi yake akijisifu kwamba nchi yake ni huru miaka 46 iliyopita.
Nawaombeni watanzania wenzangu hii nchi ni yetu sote, tugawane kidogo tunachopata kwa pamoja, walio juu washikeni mkono wenzenu walio chini tuvuke pamoja hapa hapa duniani tunapita tu hakuna atakayeishi milele sasa kwa nini umnyime haki mwenzako? tena haki za msingi? (elimu, afya na makazi) wakati wewe (serikali) ndiyo umepewa mamlaka ya vitu vyote vilivyomo ndani ya nchi hii uviangalie?
Tafakari ndugu Mtanzania mwenzangu - Utaifa mbele. Narudia Mabadiliko ni lazima.