Common Carp, samaki asiye wa asili wa Ziwa Naivasha

Common Carp, samaki asiye wa asili wa Ziwa Naivasha

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Oya nyie,wangapi wanamjua samaki huyu? Common carp!


Kwa mujibu wa madai ya baadhi ya wavuvi, samaki huyu alitoka nchini Australia na kufika Ziwa Naivasha wakati wa mvua za El Niño mnamo mwaka wa 1998.

Leo, Common Carp ni sehemu ya uvuvi na chakula kwa baadhi ya wakazi wa Naivasha lakini uwepo wake pia umeibua mjadala kuhusu athari zake kwa samaki wengine.
Kuna madai kwamba Common Carp hula Tilapia wadogo pamoja na mayai yao. Aidha, katika baadhi ya nchi inadaiwa huondolewa ikiwa bado wachanga ili kuzuia kuongezeka kwake na kuathiri samaki wa asili.

Cha kuvutia zaidi? Licha ya kuwa na mifupa mingi kuliko Tilapia na Catfish, baadhi ya wakazi wa Naivasha wanaendelea kuiona kama kitoweo.

Kwa wavuvi na wakazi wa Naivasha: Mmeona Common Carp ikiathiri samaki wengine katika ziwa?

Na kwa wale mnaowahi kula, ladha yake ikoje ukilinganisha na Tilapia?

(📹Kwa hisani ya Brygettes Ngana)
 
Back
Top Bottom