Maana ya neno "unyambulisho" ni kurefusha kitu au jambo. Mathalani, katika uundaji wa maneno, Rubanza, Y. I. (1996:90) anasema unyambuaji ni upachikaji wa mofimu [[FONT=&]kipashio kidogo kabisa chenye uamilifu (kazi) wa kimuundo na kimaana katika maumbo ya maneno[/FONT]] katika mzizi wa neno. Kwa mfano baadhi ya maneno: som-o, som-an-a, som-esh-a, som-e-a na som-w-a. Hapa umenyambua mzizi "som-".
Nadhani neno "analysis" linamanisha mchanganuo. Kwa sababu, kinyume cha neno changanya ni changanua. Kwa mfano, tunapofanya "analysis" unajaribu kuvunjavunja kitu kizima au jambo zima moja kuwa vipande vipande au sehemu sehemu. Mathalani, unapojaribu kuchanganua dhana ya "utandawazi" utaangalia fasili ya istilahi yenyewe, mambo chanya na hasi ya utandawazi na kisha kuhitimisha kwa pengine kutoa maoni yako.
Nadhani Ujerumani utaniunganisha mara baada ya mimi kumaliza chuo July, 2013