Common Errors: where do you position yourself?

Common Errors: where do you position yourself?

Keen

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2007
Posts
617
Reaction score
170
Mara kwa mara nimekuwa nikisikia watu wenye elimu mpaka hata degree holders wakisema kwa mfano: "fulani ni Lecture wa chuo kikuu" au "yule dada amesoma B.Sc. Forest" au "yule kaka ni Archictecture", etc. Nimeleta uzi huu kwa sababu wiki iliyopita nilimsikia Mtangazaji wa kituo kimoja cha TV alikuwa anaendesha kipindi wakati wa kumaliza kipindi akasema "...nilikuwa naye (jina) ambaye ni Lecture wa chuo kikuu cha Dsm,..." Niliona ni bora angeongea maneno yote kwa kiswahili. Where do you position yourself?
 
Hayo ni makosa ya kuchanganya lugha ambayo hata wewe umeyafanya kama huyo mtangazaji. Swali umeuliza kwa Kiingereza wakati maelezo unayatoa Kiswahili. Lipo neno la Kiswahili la "lecturer" yaani mhadhiri - ambalo naamini kabisa unalijua wewe mwuliza swali. Hakuna haja ya kuchanganya lugha mbili wakati kila moja inajitosheleza kimsamiati kulingana na matumizi ya wahusika.
 
Mkuu 8691jakigili umenena vyema lakini maana yangu siyo kuchanganya maneno kiswahili na english isipokuwa matumizi sahihi ya maneno ya english. Kaso wanalolifanya baadhi ya watu ni kusema fulani "lecture" badala ya lecturer kama ulivyoandika hapo juu au fulani ni "architecture" badala ya architect, etc. Hiyo ndiyo ilikuwa point yangu na siyo kuchanganya lugha.
 
Last edited by a moderator:
Nimekupata! Shida ya mtangazaji ni kushindwa kuelewa matumizi sahihi ya aina za maneno (k.m. vitenzi, nomino, vivumishi, vielezi, n.k.), na kupachika au kutamka vema. Nakubaliana na wewe kabisa!!! " Lecture wa chuo kikuu cha Dsm" ingekuwa bora aweke nomino "lecturer" ikavumishwa na kirai "wa chuo kikuu" na kuhitimishwa na kikundi kihusishi "cha Dsm."
 
Nimekupata! Shida ya mtangazaji ni kushindwa kuelewa matumizi sahihi ya aina za maneno (k.m. vitenzi, nomino, vivumishi, vielezi, n.k.), na kuyapachika mahali pale. Nakubaliana na wewe kabisa!!! " Lecture wa chuo kikuu cha Dsm" bora angetamka nomino "lecturer" ikavumishwa na kirai "wa chuo kikuu" na kuhitimishwa na kikundi kihusishi "cha Dsm."
 
Nimekupata! Shida ya mtangazaji ni kushindwa kuelewa matumizi sahihi ya aina za maneno (k.m. vitenzi, nomino, vivumishi, vielezi, n.k.), na kupachika au kutamka vema. Nakubaliana na wewe kabisa!!! " Lecture wa chuo kikuu cha Dsm" ingekuwa bora aweke nomino "lecturer" ikavumishwa na kirai "wa chuo kikuu" na kuhitimishwa na kikundi kihusishi "cha Dsm."

Mkuu 8691jakigili inaonekana wewe ni mtalaam sana wa lugha ya kiswahili!! Unafaa ukafundishe kiswahili chuo kimoja nchini ujerumani. Nimependa unyamburisho wako, neno unyamburisho ni kiswahili sahihi kweli cha analysis?
 
Last edited by a moderator:
Maana ya neno "unyambulisho" ni kurefusha kitu au jambo. Mathalani, katika uundaji wa maneno, Rubanza, Y. I. (1996:90) anasema unyambuaji ni upachikaji wa mofimu [kipashio kidogo kabisa chenye uamilifu (kazi) wa kimuundo na kimaana katika maumbo ya maneno] katika mzizi wa neno. Kwa mfano baadhi ya maneno: som-o, som-an-a, som-esh-a, som-e-a na som-w-a. Hapa umenyambua mzizi "som-".

Nadhani neno "analysis" linamanisha mchanganuo. Kwa sababu, kinyume cha neno changanya ni changanua. Kwa mfano, tunapofanya "analysis" unajaribu kuvunjavunja kitu kizima au jambo zima moja kuwa vipande vipande au sehemu sehemu. Mathalani, unapojaribu kuchanganua dhana ya "utandawazi" utaangalia fasili ya istilahi yenyewe, mambo chanya na hasi ya utandawazi na kisha kuhitimisha kwa pengine kutoa maoni yako.

Nadhani Ujerumani utaniunganisha mara baada ya mimi kumaliza chuo July, 2013
 
Maana ya neno "unyambulisho" ni kurefusha kitu au jambo. Mathalani, katika uundaji wa maneno, Rubanza, Y. I. (1996:90) anasema unyambuaji ni upachikaji wa mofimu [[FONT=&]kipashio kidogo kabisa chenye uamilifu (kazi) wa kimuundo na kimaana katika maumbo ya maneno[/FONT]] katika mzizi wa neno. Kwa mfano baadhi ya maneno: som-o, som-an-a, som-esh-a, som-e-a na som-w-a. Hapa umenyambua mzizi "som-".

Nadhani neno "analysis" linamanisha mchanganuo. Kwa sababu, kinyume cha neno changanya ni changanua. Kwa mfano, tunapofanya "analysis" unajaribu kuvunjavunja kitu kizima au jambo zima moja kuwa vipande vipande au sehemu sehemu. Mathalani, unapojaribu kuchanganua dhana ya "utandawazi" utaangalia fasili ya istilahi yenyewe, mambo chanya na hasi ya utandawazi na kisha kuhitimisha kwa pengine kutoa maoni yako.

Nadhani Ujerumani utaniunganisha mara baada ya mimi kumaliza chuo July, 2013

Kiswahili kigumu, no wonder vijana wengi wanapa F ya kiswahili. Unasomea degree ya kiswahili mkuu?
 
Kiingereza (major) na Kiswahili (minor). Kanuni za lugha zinashabihiana kwa sehemu kubwa, unaposoma lugha moja ni sawa na jiwe moja kugonga ndege wawili kwa wakati mmoja!!
 
Back
Top Bottom