company registration msaada

company registration msaada

Ngamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2013
Posts
750
Reaction score
151
naomba msaada tokwa kwa wajasiliamari wote
ningependa kujua garama za kufunngua/kusajiri company limited by share(garantee), process yote
i will apreciate it very much kwa mchango wowote ntakaopa
 
ni kama inawezekana to do it online kama paper work zote ziko sawa if yes please include a link to where i can do that
 
Na mimi ningependa kufahamu, wadau fungukeni zaidi
 
HATUA ZA UFUNGUZI WA KAMPUNI TANZANIA:
1.Hatua ya kwanza unatakiwa kuandika barua ya kuomba mamlaka ya usajili wa makampuni(BRELA) kufanya uangalizi kama kampuni unayohitaji kuifungua haina mmiliki mwingine mwenye jina kama unaloomba kwa kuandika majina matatu ukiomba kufanyia uangalizi(company check).
2.unatakiwa kuandaa kitu kinachoitwa Memorundum of Association kwa kuambatanisha nakala tatu za docs hizo baada ya kupitishwa jina la kampuni unayohitaji kufungua.
3.unaipeleka kwa wakili kwa minajili ya kuipitisha na kuisaini mbele ya wamiliki wa shares na kiasi cha mtaji uliomo katika waraka wenu(memorundum).
4.Unajaza fomu utakayo iambatanisha na Memorundum yako kwa kuipeleka BRELA kwa ajli ya malipo ya kampuni yako.
5. Malipo ya kampuni huwa yana rank katika viwango tofauti tofauti kulingana na mtaji:
(a)Mtaji unaoanzia kiasi cha Milioni moja Tshs mpaka milioni kumi Tshs ni Laki mbili.
(b) Mtaji unaoanzia kiasi cha Milioni kumi Tshs mpaka milioni Therathini Tshs ni Laki tatu.
(c) Mtaji unaoanzia kiasi cha Milioni Therathini Tshs na kuendelea hulipiwa kiasi cha Laki nne Ths.
6.Utasubili kwa siku kadhaa kabla ya kwenda kuchukua cheti chenu cha uthibiticho wa kampuni kinachoitwa certificate of registration pamoja na kopi za memorandum zenu kabla ya kwenda kwenye mamlaka nyingine kama TRA kwa usajili wa biashara yako na kupatiwa namba ya mlipa kodi,Tax Identification Number (TIN) na idara mbalimbali kwa kupatiwa leseni ya uthibirtisho wa biashara unayoifanya..
NOTE:
Viwango vya ada vilvyoorodheshwa hapo juu havipo fixed vinaweza kupanda au kupungua.
 
Shukrani mkuu,MEMORANDUM OF ASSOCIATION ni sawa na katiba ya kampuni husika,inaeleza mambo mbalimbali kuhusu kampuni zikiwemo taratibu mbalimbali za uendeshaji wa kampuni. Kama nimekosea nomba nirekebishe mkuu
 
Angalia website yao BRELA

Blera hakuna tatizo, tabu ukienda TRA, kuna wapenda rushwa wasokuwa na akili. All the Best
 
shukrani mkuu,memorandum of association ni sawa na katiba ya kampuni husika,inaeleza mambo mbalimbali kuhusu kampuni zikiwemo taratibu mbalimbali za uendeshaji wa kampuni. Kama nimekosea nomba nirekebishe mkuu

upo sawa kiongozi wala hujakosea.Mambo si magumu sana fuata hiko nlichokuandikia maana ndio procedure nlizofuata baada ya kufungua baadhi ya kampuni zangu.Gud luck brother.
 
Unataka Limited Shares in Capital au Limited Shares by Guarantee? Maana zinatofauti ndogo katika usajili wake.....hasa namna memart inavyoandaliwa!
 
Back
Top Bottom