Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa money purchasing power ambacho kinabainisha kuwa, unaweza ukakuta mshara wa Daktari wa Kenya una uwezo wa kununua bidhaa ndani ya soko la Kenya, unazidiwa na ule wa daktari wa Tanzania ndani ya soko la Tanzania. Kwa mfano, mkate Kenya tuseme unaweza kuwa unauzwa KShs 200/= na Tanzania unauzwa TShs 1,500/= Kwa hapa tu unaweza kuona kuwa mkate wa Kenya unagharimu sawa na Tshs 4,000/= za Tanzania. Kwa hiyo kwa kuangalia nominal figures, huwezi ku-rule outright kwamba mshahara mkubwa wa Kenya una maslahi kuliko ule mdogo wa Tanzania, except tu kama huyo anayepata mshahara huo Kenya, atakuwa anaishi Tanzania na kutumia bidhaa za Tanzania. Kama anaishi Tanzania hapo sawa mshahara wake utakuwa una maslahi kuzidi wa mtanzania, lakini kama Daktari wa Tanzania anaishi Tanzania na wa Kenya naye anaishi Kenya, usishangae hiyo mishahara ikawa iko sawa, au hata ule unaouona mdogo, ukawa una purchasing power kubwa kuliko ule mkubwa wa nchi nyingine.
By the way, ulishagundua kuwa kadri currency ya nchi inavyozidi kuwa na thamani ukilinganisha na Dollar, ndivyo kadri bidhaa za nchi hiyo zinavyozidi kuwa expensive and vice-versae? Kwa mfano, Euro inavyozidi ku-appreciate against Dollar ndivyo kadri bidhaa ndani ya soko la EU zinavyozidi kuwa ghali na maisha ya mtu mmoja mmoja kuwa magumu, though uchumi wa EU kwa ujumla unaweza kuwa unazidi kuimarika. Watu wanaoishi kwenye vi-inchi amabvyo currency yake ni dhaifu ukilinganisha na dola, bidhaa zao ziko cheaper, japo macro level (uchumi wa nchi ) ndiyo unakuwa mgogoro. Kwa hiyo at micro-economics level, currency ambayo ni hafifu against Dollar huwa inaashiria bidhaa rahisi ndani ya soko la nchi husika, na uchumi dhaifu wa nchi (marcro-economics level) katika ujumla wake, and the vice-versa is true!