Competitive Programming

Competitive Programming

Drone Camera

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Posts
14,041
Reaction score
13,907
Hello Geeks!
Leo tuongelee huu uwanja wa tech kama kichwa kinavyoeleza.
Naamini kila mmoja anajua maana ya programming.Kwamba unaandika instructions katika computer(programs) ili iweze kukupa matokeo unayotaka wewe. Ila kwa upande wa "Competitive programming" ni kwamba utafanya hiyo hiyo programming ila kwa upande wa ushindani. Kwa maana nyingine, utatumia skills zako hizo kutoa ushindani kwa watu wengine.
Na sio kushindana tu, unaweza ukafanya competitive programming ili kujiimarisha zaidi katika uwanja wa teknolojia.
Tumekuwa tukitoa sifa sana kwa programmers wa nchi zilizoendelea kwamba wametuacha mbali katika sekta hiyo huku tukisahau kuangalia misingi waliyojijengea ili kufikia huko.Ni kwamba wengi walifanya competitive programming walipokuwa wanasoma either high school au chuo kikuu na wengine bado wanafanya hata sasa wakiwa makazini kwao.
Kuonyesha kwamba hili swala sio la mzaha makampuni makubwa ya tech duniani wana mashindano yao binafsi ya competitive programming ili kupata watu watakaoweza kuongeza kitu katika kampuni zao. Mfano google wana CodeJam na Kickstart. Facebook wana HackerCup. Kuna pia ICPC, haya ni mashindano makubwa kabisa kwa wanafunzi wa university.
Faida nyingine ya muhimu sana ni kwamba kwa mtu aliyefanya competitive programming kama anataka asome kitu kingine upande wa tech basi itamchukua muda mfupi sana kulinganisha na mtu asiyefanya kabisa.Pia utakuwa na strong problem solving skills pamoja analytical skills ambazo ni muhimu ili kuwa software engineer mzuri.
Hauhitaji kuwa guru ili uanze.Unachohitaji ni basic knowledge ya data structures na algorithms.Mengine utajifunza kadri unavyoendelea.Chagua programming language moja tu unayoipenda hauhitaji kujua zote. Zinazopendekezwa ni C++, Java na Python kwa mpangilio huo.Na hauhitaji uwe expert wa language fulani utakayoichagua ili uanze.Soma basics na syntax kisha ujue kuitumia kuandikia basic data structures na algorithms.
Uzuri ni kwamba kwa sasa kuna online platforms nyingi unazoweza kuanzia muda wowote.Kuna Hackerrank, HackerEarth, na nyingine nyingi.
Nakuomba sana kama wewe ni mwanafunzi upande wa IT kama Computer Science, Engineering n.k au kama ni mpenzi wa tech basi uanze kuangazia huu upande kwa sasa.
Kikubwa kinachohitajika ni bidii yako, focus yako na malengo thabiti.Bye for now✋
 
Back
Top Bottom