Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Asante kwa somo hilo hapo juu
Nimelipenda
Mukulu,kabla ya kwenda kote huko,unaweza kutembea barabarani na ukaona "nyayo" na ukaanza kujiuliza "kuna nini kimepeta hapa"
Hilo aina la swali linaashiria kuwa "unadhani" kuna kilichopita hapo lakini bado hujajua ni nini
Sasa basi,duniani kuna uhai na viumbe hai ambavyo vina utaratibu na maumbile tofauti,kwa mantiki hiyo hapo juu ya "nyayo",huoni kwamba kuanza "kudhani" kuwa kuna aliyefanya haya yote ni sahihi kimantiki badala ya kuanza kudhani hakuna aliyefanya? [kabla hata ya kuamua kuwa aliyeyafanya haya ni Mungu]
Kwa nini usitumie Mantiki itakayokufanya udhani kuwa "nyayo" ni za "kitu" kilichopita hapa kwenye suala la kuonya "nyayo" kama binadamu,miti n.k kuwa ni alama ya uwepo muwekaji?
Mukulu,unaamini leo tena?
Halafu kwanini unadhani kuna contradiction?
Basis za contradiction ambazo zinakufanya "uziamini" na kuzitumia kwenye mambo ya Mungu uliyoyasikia zimetoka wapi?
Kwanini hazibadiliki?
By the way,ni contradiction au hujaelewa?
Kwa nini sababu ya uhai na dunia kuwapo iwe ni "nani" na si "nini"?
Mungu mwenye uwezo wote, upendo wote, ujuzi wote kwa nini aachie viumbe wake aliowaumba mwenyewe na anaowapenda wapate maumivu, magonjwa na mabaya yote ya dunia hii wakati ana.kila uwezo na sababu ya kuzuia hilo?
