Compliant

Compliant

stev30sudi

Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
45
Reaction score
17
Inakuwaje gari au pkpk linapokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi, ndani ya siku chache tu hung'olewa vifaa<spea> palepale Kituoni? Mmilki amdai nani uharibifu huo kwani hakuna uhusiano wa kosa lilimfikisha pale na kuingizwa hasara ya mali kwa Uzembe au kukosa uaminifu kwa Watendaji Serikalini?
 
Unastahili kulipwa lakini ni sharti uchukue hatua za kudai haki yako
kumbuka hakuna haki utakayoletewa kwenye kisahani...
Mwone mkuu wa kituo au OCD au RPC
AU andika demand letter/note kwa Mkuu wa kituo mnakilie Ocd, Rpc na hata IGP
Pia waweza kufuata taratibu zilizoainishwa katika Government Proceedings Act kulishitaki jeshi la Polisi
Kumbuka kabla hujaruka mto agana na nyonga zako kwanza...hakikisha unao ushahidi wa kutosha kuhusu
madai yako kabla ya kuchukua hatua yeyote vinginevyo yaweza kula kwako...
Onana na wakili/mwanasheria aliyekaribu nawe akushauri
 
Back
Top Bottom