Computer za ushahidi zilizotumika kwenye uwizi wa atm zaibiwa ndani ya kituo cha polisi - makao maku

Computer za ushahidi zilizotumika kwenye uwizi wa atm zaibiwa ndani ya kituo cha polisi - makao maku

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
COMPUTER ZA USHAHIDI ZILIZOTUMIKA KWENYE UWIZI WA ATM ZAIBIWA NDANI YA KITUO CHA POLISI - MAKAO MAKUU MWANZA




Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM).


Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.



Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.



Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.



Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.

COMPUTER ZA USHAHIDI ZILIZOTUMIKA KWENYE UWIZI WA ATM ZAIBIWA NDANI YA KITUO CHA POLISI - MAKAO MAKUU MWANZA - MPEKUZI HURU
 
Jeshi la polisi siku hizi ni aibu ya nchi..
 
In this veeere lovely country of oursn everything is business. You can even buy police security for your family to ensure a goodnight sleep. Kuna this house ipo masaki mtaa wa chole, sio ya diplomat wala m2 mwenye wadhifa serikalini lakin huo ulinzi wa polisi usiku pita karibu uone. Nshawahi pewa kesi ya uzururaji na uzembe
 
Na ndiyo hawa hawa wanatumiwa na pinda kuwapiga watanzania wanao lilia haki zao!?
 
Back
Top Bottom