Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CONDENSTER SICHALWE AISHAURI SERIKALI KUANZISHA WIZARA MPYA "WIZARA YA TEKNOLOJIA"
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technologia ya Habari ameishukuru Serikali kwa kujenga Minara ya Mawasiliano katika Kata ya Momba
"Tunaomba kuendelea kuboreshewa Minara kwenye Kata za Kapele na Kitete sambamba na kuhakikisha mnatuchepushia Mkongo wa Taifa kufika Makao Makuu Chitete. Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technologia ya Habari imebeba ajira nyingi sana za vijana kama ukiamua kutumia Teknolojia kwa mlengo chanya" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
"Tunaomba tupate Wizara mpya ya Teknolojia ili tuweze kuendana na Karne ya Ishirini na Moja ili tuendane na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolutions). Hakuna namna tunaweza kulikwepa jambo hili maana ndiko wakati unapotupeleka" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
"Ilani ya CCM 2020-2025 sura ya Nne inasema Sayansi, Teknolojia na Ubunifu uk. 154 - CCM inatambua kuwa Uchumi wa Kidigitali ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa kuongeza ufanisi katika uzalishaji na utekelezaji wa shughuli mbalimbali na kutoa fursa za kuongeza vipato kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Uchumi huo umeonekana kuwa eneo muhimu katika kuchangia kukuza uchumi nchini kama ilivyofanyika katika nchi zingine za kupato cha kati. Aidha, Uchumi wa Kidigitali unalandana na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolutions) yanayokuja na ambayo hayaepukiki. Hivyo basi, CCM itaendelea kuisimamia Serikali kuhakikisha kuwa Teknolojia mpya za kidigitali zinatumika kuongeza ufanisi katika sekta za uzalishaji na kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
"Katika kipindi cha Miaka mitano ijayo, CCM kinaelekeza yafuatayo; Kuimarisha kituo cha utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa TEHAMA ikiwemo kujenga uwezo wa kuongeza matumizi ya Teknolojia mpya ya kidigitali" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
"Yupo msanii Diamond Platinum, muulize ameshapeleka kazi zake kwenye NFT? Bado. Ni msanii wetu inabidi tulinde kazi zake ili kazi zake zisije kupata madhara. Ni muhimu zaidi kwa Wasanii na waigizaji wetu" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
"Tunatamani kuona Teknolojia tunazozipata zisiende tofauti na kazi zetu tunazozifanya na taratibu tulizojiwekea kwenye nchi yetu. Kama kungekuwa na utafiti tungejua namna ya kuitumia PayPal kama ni njia ya kulipa na kulipwa. Watanzania walipa kwa PayPal kupitia Kenya kwa nini siyo Tanzania?" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe
"Block Chain Technology siyo Teknolojia ya kuidharau maana ni Teknolojia yenye mawanda mapana. Ndani ina mambo ya Sheria, Mikataba, NFT (Wasanii ). Block Chain pekee inaweza kuzalisha ajira nyingi sana kama ilivyoelezewa kwenye Ilani ya CCM" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe
"Wapo ma professor Tanzania ambao wameandika maandiko kadhaa kuhusu Block Chain Technology. Waziri ukae nao ili Jamii ijue. Block Chain Technology itaambatana na changamoto nyingi ambazo hatuwezi kuziepuka" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe
"Waziri kaa na timu yako pitia kuhusu Coin Market Cap. Waziri boresha utafiti kama ambavyo Ilani ya CCM 2020-2025 inavyosema. Kama itawapendeza Serikali Tunaomba tupate Wizara mpya yaani Wizara ya Teknolojia" - Mhe. Condenster Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba