Confession about wauza mihogo coco beach

Confession about wauza mihogo coco beach

Salaam wana jukwaa.

Nimepita sehemu moja nikakuta watu wanajadili kuhusu tabia ya upigaji ya wauza mihogo na mishikaki COCO BEACH.

Malalamiko yamekuwa mengi kuhusu tabia yao ya kuuza mishikaki kwa bei ya juu huku bidhaa hizo zikiwa sio za gharama hiyo kwa uhalisia.

Sasa kama wanajamvi naomba tusaidiane namna ya kukabiliana na wahuni hawa.

Tupatie mbinu ya kuhakikisha hauingii kwenye upigaji wa hawa jamaa.
Nami napenda kujifunza hayo maneno "confession about" imekaa kwenye kichwa cha habari yakimaanisha nini?
NB;Sijawahi kufika Coco beach sijui wanavyopiga mahela.Karibu kijijini Ntalikwa hapa Tabora upate mbowoto na nsansa kwa bei nafuu.
 
"Ushuhuda kuhusu"
 
Back
Top Bottom