Elections 2010 CONFIRMED: Kigwangala atangazwa rasmi mshindi Nzega

Kiranga ulishawahi kugombea Ubunge hata mara moja au we kazi yako ni kukosoa wenzako walioonesha dhamira ya kuwatumikia wananchi? Ushawahi hata kuzunguka kupiga kampeni kutafuta kura???

I advise you to shut up on things greek to you! Its also wisdom...

Huwa ninaamini kuwa wengi wa waliopo hapa ni wasomi wazuri tu na mnafahamu maana halisi ya uhuru wa kutoa maoni, wa kuchagua n.k. Lkn to my surprise mtu anadhani itikadi yake ya chama ndiyo sahihi zaidi ya wengine na mara zote anatukana tu wengine kwa kuwa wana itikadi tofauti na ya kwake! That is not democracy!
 

Bwe he he he..
 

Dr;

Wewe ni Mbunge nakushauri uwe unachagua kwa uangalifu sana vitu vya kujibu na sikushauri kabisa kuwa uwe unajibu kila tuhuma zinazo elekezwa kwako!

By the way; Dr umetoa tamko lolote officially hadi sasa la kuwashukuru wapiga kura wako kwenye"bahati"yako ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Nzega?
 
Kiranga ulishawahi kugombea Ubunge hata mara moja au we kazi yako ni kukosoa wenzako walioonesha dhamira ya kuwatumikia wananchi? Ushawahi hata kuzunguka kupiga kampeni kutafuta kura???

Huyu katika fikra zake zote anafikiri njia pekee ya "kuwatumikia wananchi' ni kwa kuwa mbunge. Yaani mawazo mgando matupu, hakuna kufikiri zaidi ya formulaic norms.

I advise you to shut up on things greek to you! Its also wisdom...

Halafu arrogant as fvck, hata hanijui, kauliza swali, badala ya kusubiri jibu "ndiyo nishawahi kugombea ubunge pale' au "sijawahi' tayari kashaconclude kwamba sijawahi, na siasa mbuzi za kugombea ubunge kutupwa kwenye party primaries, na kushinda kwa bahati sizijui.

Huwa ninaamini kuwa wengi wa waliopo hapa ni wasomi wazuri tu na mnafahamu maana halisi ya uhuru wa kutoa maoni,

Kama kweli unaamini moja ya alama za usomi ni kuthamini uhuru wa kutoa maoni, wewe mwenyewe ushaji disqualify kutoka kundi hili la wasomi kwa kuniambia "shut up". Huwezi kutaka kuwanyamazisha watu kwa nguvu halafu hapo hapo ukajitia bashasha za usomi na kuthamini uhuru wa watu kujieleza.

wa kuchagua n.k.

Ungekuwa kweli una principles za kuthamini uhuru wa watu kuchagua ungekataa nomination ya CCM, kwa maana wanachama wa CCM hawakukutaka uwe mgombea wao, hawakukupa hata nafasi ya pili kwenye kura zao za maoni, wamekutupa a distant third. Leo unataka kutuhubiria kuhusu kuthamini haki ya wananchi kuchagua hapa ?

Lkn to my surprise mtu anadhani itikadi yake ya chama ndiyo sahihi zaidi ya wengine na mara zote anatukana tu wengine kwa kuwa wana itikadi tofauti na ya kwake! That is not democracy!

Itikadi ya chama gani? Mimi nina itikadi ya chama gani? Angalieni huyu simpleton anaamini kwa kuwa yeye CCM basi anayetaka kumuwajibisha lazima atakuwa na itikadi ya chama tofauti.

Wengine hatuna chama hapa, chama chetu hakijatokea bado ktika nyanja za siasa Tanzania, in the meantime tunawashikisha adabu arrogant nincompoops kama wewe wanaofikiri wamepata ubunge kwa nguvu zao wakati wamebebwa mpaka inatia kichefuchefu.
 
Murder-matchetering..lolz

Ngoja niwashe coffee maker..Mhhh..
 
hongera sana,inafurahisha kuona vijana wenzetu wanaenda mbali katika kulijenga taifa na tunaamini na wewe utakuwa mwakilishi wetu mzuri bila kuweka tofauti za kisiasa na nimependa confidence yako omethubutu kuingia jamvini bila kujificha na kutetea hoja,yo are the man.

Ndio mtuwakilishe vizuri huko na Mungu akutangulie wewe na wabunge wote vijana wawe ccm,shadema cuf,nk..maana huko tunakoenda tunahitaji vijana waliokomaa kisiasa wazee watapita tunataka damu mbichi amabao ni wachache.

All the best

:hippie:
 

Tumpe astahilicho kupigiwa kura si mchezo na ku-chapa barua si ufahari hakuna masharti ya kuweka mara dole gumba space mbona ww Gaijin huna herufi kubwa katika sentensi zako tumia shift URAIS UDIWANI UBUNGE hausomewi popote au huijui CCM CHAMA TAWALA HONGERA DR KUSHINDA JIMBO LA NZEGA ukiwa nyuma ya BASHE NA MPIGANAJI WA MAFISSADI
 
Pole sana Kiranga, nisamehe, naona nimekukwaza! Sorry pal.

@malafyale, nishawashukuru wanaNzega kwa kuniamini, and have done so several times and will do so in every ward!

To set records straight, 'bahati' ni ile niliyoipata kwa kuteuliwa na chama changu baada ya kuwa 2nd runner up kwenye primaries - to me that seems like pure luck plus the fact that chama kiliamini nitakipa ushindi kwa kuwa nina sifa na wasifu stahiki wa kuwa MB, kushindwa kwenye kura za maoni is a function of so many things, sipendi kusema hapa sababu hizo!

Wengi ndani na nje ya CCM, they thought Kigwangalla hauziki na atashindwa kwenye general election, lakini mi na wanaccm wenzangu persevered and fought hard to win the election! Hii sasa haikuwa 'bahati' ni ushindi tulioutafuta kwa sera nzuri za chama na confidence ya uwezo wa kufuatlia na kusimamia utekelezaji, ya wagombea wa CCM, hususan Mbunge wao! Ikafika mahali wakaamini, wakanipa kura nyingi!
 
I think your a good person hongera ILA CHAMA CHA MAJAMBAZI mhhhhhhhh!!!
 
Mimi nafikiri tusimshambulie Hamisi

Tumpe Muda atuthibitishie kweli ni Mzalendo wa kweli , mpigania haki za wananchi
tusubiri kumpima kwa hoja zake bungeni na utendaji kazi wake jimboni

Ni kijana aliyethubutu , mwenye mawazao ya kimapinduzi

Japo siishabikii CCM lakini sioni sababu ya kumchukia na kumponda kila MwanaCCM

Asalaam Aleikum
 

Kama ulichakachua na wewe nenda kafanye toba kabisaa
 
Mkuu. Statements zako na majibu yako yanazidi kunikatisha tamaa. Ulivyomjibu Kiranga kunaonyesha arrogance na immaturity. I hope you will prove me wrong katika utendaji wako.

Amandla.....
 
Hata kama kashinda nadhani the time will tell us kwamba ni hodari kiasi gani katika kutetea hoja muhimu bungeni Huenda kura za maoni wenzake walichakachua maana ameshinda kwa kura nyingi za uchaguzi mkuu
 

Vipi nguvu za ziada hazikutumika huku Nzega?
 
@ahsante Henge na tanzActive. Sintowaangusha wanaNzega na waTz wenzangu

@Tom Odera, surely let's wait for time to tell us...why the pessimism?

@fundi mchundo, am never arrogant and ofcoz am young but wise and hardworking!

@hisia kali, hakuna nguvu za ziada zilizotumika Nzega, that was a clean win!
 

Tupo pamoja
Ule moto wa MUCHS uende nao bungeni
ukiwa kibaraka utavunja nguvu sana tunakufamu na utaporomoka kwa umashuhuri kama Kikwete
huo ndo ushauri wangu
 

Mheshimiwa Naomba nikupe Hongera sana kuchaguliwa kwako kutokana na sera nzuri za Chama chako kama ulivyo sema, Mimi naomba unieleze sera nzuri za CCM za Uchaguzi Huu maana mimi nilikua sisikii sera bali nikikua nasikia Ahadi nyingi tu Kuanzai Kwa JK, sasa na wabunge walikua wanaendeleza zile ahadi alizo zitoa Mheshimiwa au mlikua mnatoa sera kama ni sera zilikua ni zipi Mheshiwa?
 

Yes, Na tunajua wamekutuma kufanya nini! Ingawa hata Bashe simfagilii, nina wasi wasi na nguvu iliyotumika kumwengua ili tu wewe upite. Sema ukweli ni vipi Bashe ajengewe zengwe vile, halafu mtu wa pili aliyewahi kuwa Mbunge wa hapo aambiwe hauziki, halafu wewe ndo ghafla uonekane unafaa?
Nakupa Hongera kwa ushindi, lakini kuna maswali magumu yasiyo na jibu.
Kama waliokuteua kwa bahati kama wewe mwenyewe unavyosema wamekuteua ili wapate mtu wa kutuletea maendeleo, hewalah, Mungu akujalie utufanyie hayo. Lakini kama wamekupitisha ili uwe boya la kuwafikisha katika pepo ya ufisadi, tutasikikitika sana na kumwonea huruma Bashe milele.
It is a matter of time before we see your true colours.
I wish you all the best, Dr, na tumia elimu yako kuprove watu walikuwa unnecessary negative!

Time will tell.....
 
Swali kwa mbunge mteule
What are your comments to what happened to Bashe?
Were you part of it?
Reconciliation and working together for development of Nzega?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…