Movic Evara
Senior Member
- Jan 31, 2018
- 197
- 431
Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umebeba historia ndefu inayohitaji muda mrefu kuielezea, lakini nitajaribu kuifupisha kwa kuangazia mambo machache muhimu.
Mpelelezi wa Kiingereza, John Speke, katika kitabu chake Journal of the Discovery of the Source of the Nile (1863), aliandika kuwa asili ya Watutsi ni Pembe ya Afrika (Ethiopia, Somalia, Djibouti), na kwamba walihama katika karne ya 12 wakielekea eneo la Maziwa Makuu. Walifanya makazi yao katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Tanganyika, eneo ambalo kwa sasa ni Rwanda, Burundi, na Congo. Walipowasili, walikuta wenyeji ambao Wahutu na Watwa, ambao waliishi nao kwa amani. Wahutu na Watwa walikuwa wakulima, huku Watutsi wakiwa wafugaji.
Wakoloni waligawa maeneo ya kiutawala bila kuzingatia kijamii iliyokuwepo, na hivyo kuna jamii zikajikuta mataifa mawili. Kwa mfano, Wamasai walijikuta Kenya na Tanganyika. Watutsi walijikuta Belgiam Congo na German East Africa (Tanganyika), wakati huo Rwanda na Burudi yakiwa majimbo ya Tanganyika.
Baada ya WWI Ujerumani ilinyang'anywa makoloni yake yote. Germanan East Africa ikagawanywa, Rwanda, Burundi wakapewa Ubelgiji kama nchi moja Ruanda-Urundi, na Tanganyika ikapewa Uingereza. Jamii ya Watutsi nayo ikazidi kugawanyika kati ya Ruanda-Urundi, Congo, Uganda na wachache Tanganyika.
Pamoja na kuwa wachache kwa idadi lakini walijikuta wamegawanyika katika mataifa tofauti ingawa walikuwa watu wa jamii moja, walioongea lugha moja, wenye mila na desturi zinazofanana.
Watutsi waliojikuta eneo la Kivu (Congo) hawakupata ushirikiano mkubwa kwa watu wa eneo hilo kama Wabembe, Wavira, na Wanyindu, kwa sababu ya kujiona wa hadhi ya juu (ubugabire). Watutsi waliojipata Congo walikua wachache, sehemu kubwa ilibaki Ruanda-Urundi.
Walishauriwa kuhamia Ruanda-Urudi, lakini hawakua wanyarwanda wala Warundi. Ni Wakongomani waliozaliwa Congo. Babu zao walifika hapo toka karne ya 12 lakini mipaka ya wakoloni illiwafanya wajikute katika mataifa tofauti tofauti.
Wale walioangukia Ruanda-Uurundi waliendelea kujiita Watutsi, walioangukia Congo hawakujiita Watutsi. Wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni.
Ni sawa na wamassai wa TZ na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza Wamasai wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania.
Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Hii ni kwa sababu walijiona daraja la kwanza kabla ya wengine (Ubugabire). Hata wakoloni walipokuja waliwatreat kama daraja la kwanza na kuwapa favors nyingi. Kwa sababu ya 'Ubugabire' hawakutaka kuchangamana sana na wenyeji, hivyo wakaongeza mwingiliano na Watutsi wa Rwanda.
Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka.
Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge).
Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.
Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF.
Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma.
Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo.
Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu.
Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja.
Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa.
Wakati hayo yakiendelea Congo, kule Rwanda, kikundi cha waasi cha RPF chini ya Paul Kagame kilifanikiwa kuyashinda majeshi ya serikali na kuchukua dola baada ya yale mauaji ya kimbari. Askari wa jeshi la Rwanda, ambao wengi walikuwa Wahutu (Itarahamwe), walikimbilia Congo. Walipofika kule, wakaanzisha kikundi cha waasi cha kupigana na serikali ya Rwanda kilichoitwa FDLR. Kikundi hicho kikaungwa mkono na serikali ya Mobutu. Hivyo Mobutu akawa anawapa silaha wapigane na serikali ya Kagame ili kurudisha utawala wa Wahutu madarakani.
Wakati Mobutu akisaidia waasi kuangusha serikali ya Rwanda, kulikia na vikundi vya waasi zaidi ya 40 vinapigana na jeshi lake. Moja kati ya vikundi hivyo ni Alliance of Democratic Forces for the Liberation (AFDL) kilichokuwa kinaongozwa na Mzee Laurent Kabila, ambaye ni Mluba wa Katanga, kusini mashariki mwa Congo karibu na Ziwa Tanganyika.
Baada ya miaka karibu 30 ya kupigana msituni, hatimaye nguvu zikapungua. Akawa haendi tena mstari wa mbele. Mara kwa mara alikuja kupumzika nyumbani kwake Msasani jijini DSM, akimuachia Kanali Reuben Um-Nyobe kuongoza kikosi msituni.
Mobutu alipoamua kuwasaidia askari wa FDLR (Intarahamwe) kupigana na serikali ya Rwanda, Kagame nae akaamua kumuunga mkono Laurent Kabila na kikundi chake cha AFDL ili wamng'oe Mobutu. Yaani, serikali ya Rwanda ikaunga mkono waasi wa Congo kwa sababu serikali ya Congo inaunga mkono waasi wa Rwanda. ‘Scratch my back, and I will scratch yours’.
Wakati huo, inadaiwa serikali ya Rwanda ilikuwa imepata silaha nyingi kutoka Ufaransa na UK, kwa hiyo Kagame alijipima akaona ana nguvu za kupigana na Mobutu. Wakati huo Kagame alikuwa Makamu wa Rais chini ya Pasteur Bizimungu, lakini yeye ndiye aliyeongoza kila kitu. Sababu za kumuunga mkono Kabila;
1. Ethnicity (Waluba na Watutsi wanaelewana)
2. Mobutu kuunga mkono FDLR (Intarahamwe)
3. Uwepo wa rasilimali nyingi sana eneo la Kivu, hasa madini.
Eneo la Kivu ni eneo la kimkakati sana na mabepari wote duniani wanalitolea macho kutokana na utajiri wake. Kivu ina madini ya Coltan ambayo yanatumika kutengeneza simu na laptop. 80% ya coltan yote duniani inatoka Congo (unaweza kugoogle kama huamini). Yani kwa kifupi bila Congo hakuna smartphones wala laptop duniani.
Kivu pia kuna madini ya tin yanayotumika kutengenezea solder za kuchomelea vifaa vya kielektroniki kama radio, TV, simu, nk. Kuna madini ya Tungsten yanayotumika kutengenezea silaha. Na pia kuna Cobalt inayotumika kutengeneza betri mbalimbali zikiwemo za magari. Kama haitoshi Kivu kuna dhahabu nyingi mno. Eneo la Kivu ni eneo lenye dhahabu nyingi zaidi duniani ambayo bado haijachimbwa (The most unexplored gold site globally).
Kagame aliona fursa. Wakati huo Rwanda ilikuwa imetoka kwenye vita na machafuko ya muda mrefu. Akataka rasilimali za jirani. Lakini atazipataje wakati yeye na Mobutu hawaelewani? Akakaamua kumuunga mkono mzee Laurent Kabila. Lakini akaweka masharti. Nikikusaidia kumng'oa Mobutu, eneo la Kivu Kusini, lenye Watutsi wengi (Banyamulenge), litajitenga na Congo na kuwa nchi inayojitegemea.
Alishapiga hesabu za mbali za kuifanya Kivu kuwa sehemu ya Rwanda baada ya kujitenga DRC. Kabila akasema poa tu. Ashapigana miaka 30 msituni bila mafanikio? Sasa kapata "kamserereko" ka kwenda Ikulu akatae? Kagame nyuma yake walikuwepo Ufaransa na Uingereza akasema twende kwa maandishi. Mkataba ukasainiwa mji mdogo wa Lemera, Kivu Kusini. AFDL ikapewa support ya silaha na pesa, ikaamsha dude kupigana na majeshi ya serikali (FARDC).
Wakati Mobutu anajaribu kupambana na AFDL, vikaibuka vikundi vingine vya waasi zaidi ya 40 kupigana na majeshi ya serikali. Vita ikiwa imepamba moto, Rwanda ikajitosa rasmi kupigana na serikali ya Mobutu kwa kisingizio cha kuwatafuta wanamgambo wa Intarahamwe waliokimbilia Congo. Uganda nayo ikaingiza jeshi kuwatafuta waasi wa LRA. Mobutu kaona "nini cha kufia" akadaka chopa akatokomea zake Moroco. Kesho yake tar.17 Mei 1997, Laurent Kabila akatangazwa Rais mpya wa Congo. Vita hii ikabatizwa jina vita vya kwanza vya Congo (1996-1997).
Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini?
Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila.
RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege.
Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza.
Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda).!