Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa bonge la msanii fulani hivi tu.Ni ile hali ya kumsikiliza bila kukusanya taarifa nyingi na sahihi
TayariTunangoja muendelezo
Good luck#PART4
Baada ya Ntaganda kupelekwa The Heague, M23 iliongozwa na Sultan Makenga, Mtutsi wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini. Mwaka 1990 Makenga akiwa na miaka 17 tu alienda Rwanda kujiunga na kikundi cha waasi RPF kilichokuwa kinaongozwa na Jenerali Fredy Rwigyema. Sultan Makenga akiwa askari wa RPF alipigana msituni dhidi ya serikali ya kihutu ya Juvenile Habyarimana.
Baada RPF ilishika dola, Askari wote wa RPF waliingizwa katika jeshi la Rwanda akiwemo Sultan Makenga. Alihudumu katika jeshi hilo kwa muda mrefu hadi kufikia cheo cha Kanali kabla ya kurudi "nyumbani" Congo, kujiunga na kikundi cha waasi cha CNDP. Baada ya mkataba wa amani wa March 23, 2009 Sultan Makenga alikuwa miongoni mwa askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo (FARDC).
Mwaka 2012 Bosco Ntaganda alipojitoa kwenye jeshi la Congo na kuunga kikundi cha waasi cha M23, Sultan Makenga alikua wa kwanza kujiunga. Baada ya Ntaganda kujisalimisha, Makenga akapewa uongozi wa M23. Akaongoza kuanzia 2013 hadi 2016 kisha akaachia uongozi na kuhamia uhamishoni nchini Rwanda. July 2024 Makenga alizungunza na media kwa mara ya kwanza akiwa Kigali na kueleza bado ana azma ya kuikomboa DRC.
Baada ya Makenga, M23 ikapata viongozi ambao hawakuwa mashuhuri hadi 2022 ilipompata Corneille Nangaa, aliyekua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi (CENI) na ndiye aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi wa December 30 mwaka 2018.
Katika mambo yanayoshangaza na kufanya vita ya Congo kuonekana ngumu, ni jinsi Nangaa alivyotoka kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hadi kuanzisha coalition ya vikundi vya waasi, Congo River Alliance (CRA) na kuingiza M23. Nangaa ndiye ameongoza M23 kuutwaa mji wa Goma January 2025, na kuyafurusha majeshi ya serikali. Nangaa ametangaza nia ya kumuondoa madarakani Rais Tshisekedi, ambaye mwaka 2018 alimtangaza kuwa Rais.
August 2024 Mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa ilimhukumu Nangaa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la uhaini. Hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo mahakamani (death sentence in absentia). Nangaa amesema ikiwa M23 itashika dola, wale waliomhukumu ndio watanyongwa kwa niaba yake.!
Itaendelea.... (popcorn zisiishe).!
Damu inamwagika ili familiya za kagame na mseven ziishi Kama peponi...hao wanajeshi nao NI wajinga wanashindwa kumtwanga kagame warudi kwao Rwanda Kama anawapenda kwa Nini haearudiahi nyumbani Kigali..wanataka Kongo isiyo yao...haaaaaaa pandora box hiii ....huu mgogoro ni mkubwa sana damu za watu zilizwamwagwa hapa hii nchii haiwezi tulia labda ikatwe iwe ndogo ndogo ila kwa ukubwa huo haiwezi tawalika
kagame ni moja ya matatizo hata yeye akifa sasa hivi hii vita haiwezi isha miaka 1000.....kuna vikundi vidogo zaidi ya 100 na nchi ni kubwa sana na maliasili ni nyingi na dunia nzima inafaidika ila wakongo ndo wanapata hasara maamuzi yafanyike kwa maslahi ya wakongoDamu inamwagika ili familiya za kagame na mseven ziishi Kama peponi...hao wanajeshi nao NI wajinga wanashindwa kumtwanga kagame warudi kwao Rwanda Kama anawapenda kwa Nini haearudiahi nyumbani Kigali..wanataka Kongo isiyo yao...
Survival for the fitnessKagame anatetea ndugu zake watutsi. Mimi naona tatizo la huo mgogoro upo sehemu mbili:
1. Watutsi/Banyamulenge wa Kongo kutopewa haki zao kama raia halali wa DRC
2. Maslahi binafsi ya nchi na makundi mbalimbali ktk eneo la Kongo mashariki mahali ambapo kuna rasilimali nyingi. Hivyo, Serikali ya Kongo isaidiwe kuunda Serikali yenye nguvu na itakayohusisha makundi yote nchini humo.
Hivi haikuwa kipindi Cha Donald CameroonMapatano alikuwa anasema mpiganaji mmoja juzi ni kwamba kwa kumuondoa Mobutu Rwanda itapewa North and South Kivu na Uganda itapewa Ituri..
Lakini kama watu wandaiana malipo kama hayo,it is something that can be estimated and calculated.
Nakumbuka wakati ule Tony Blair alipokuwa Waziri Mkuu siku moja ilitangazwa," Leo Uingereza imelipa installment ya mwisho ya deni lake kwa USA kwa msaada iliopata WW2"
Noma sana!Nkunda anazuiliwa Rwanda,Bosco Ntaganda anatumikia kifungo the gauge
Kwamba mwisho wa siku Pk anashindwa kuwasaidia watu wanaompasupport kupgana na Congo
Kwa hisia rahisi tu, Kagame anahusika kwa sababu asipofanya hivyo, walw Banyaamulenge wakifurushwa huko Mashariki ya DRC watarudi Rwanda wakati ardhi ni ndogo. Kagame anaendelea kuwapambania wabaki huko huko DRC ili angalau hata awe anawatumia kupata chochote kitu madiniHalafu anakuja mtu ameshiba makande anakwambia Kagame hahusiki. Nimempuuza sana PLO Lumumba
Noma sanaCONGO CRISIS - PART 3
Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda.
Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake:
- Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo.
- Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo.
- Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994.
Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege).
CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo.
January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi, mzaliwa wa Kinigi, jimbo la Musanze nchini Rwanda akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini.
Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwao "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo:
- Kusitisha mapigano kwa pande zote.
- Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo.
- Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita.
- Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao
- Kulinda haki za binadamu Kivu.
March 23, 2009 Mkataba ukasainiwa huko Goma, kati ya serikali ya Congo na Waasi wa CNDP, wasuluhishi wakiwa mzee Mkapa na mzee Obasanjo. Mapigano yakasitishwa.
Ntaganda na askari wa CNDP wakaingizwa kwenye jeshi la Congo (FARDC). Kukawepo na miaka mitatu ya amani, vita ikakoma kabisa. Lakini ghafla, April 04, mwaka 2012 Bosco Ntaganda alitangaza kujitoa kwenye jeshi la Congo (FARDC) pamoja na baadhi ya askari waliokuwa wanamgambo wa CNDP. Ntaganda alidai Serikali ya Congo imeshindwa kutekeleza mkataba wa amani wa Machi 23, 2009.
Alisema Makataba huo uliweka masharti ya kutowabughudhi askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo. Lakini serikali ya Congo iliwashughulikia. Baadhi walikamatwa na wengine kuuawa. Pia alidai serikali ya Congo imeshindwa kuwalinda Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo.
Ntaganda akatangaza kuanzisha kikundi kipya cha waasi kiitwacho M23. Alidai kutumia jina hilo ili kuikumbusha serikali ya Congo kuheshimu mkataba wa amani wa Machi 23, 2009. Kundi la M23 likapata wafuasi wengi hasa askari wa zamani wa CNDP na Banyamulenge wa Kivu. Mapigano yakaanza upya.
Rwanda na Uganda zikashutumiwa kuunga mkono waasi hao, lakini zikakataa. Hata hivyo Rwanda ililaumiwa kwa kuruhusu M23 kuwa na kambi za kijeshi katika miji ya Gisenyi na Rusizi. Pia Rwanda ilihusishwa na mgogoro huo kwa sababu Ntaganda hakuwa Mkongomani, bali Mnyarwanda aliyezaliwa na kukulia Rwanda. Ametumikia jeshi la Rwanda kwa miaka mingi, kabla ya kuhamia Congo kupigania haki za Banyamulenge.
Baada ya mwaka mmoja wa mapigano makali, vikosi vya M23 vikazidiwa nguvu na jeshi la serikali. Machi 18, 2013, Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda na akaenda mwenyewe kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali. Akasafirishwa kwenda The Heague kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC).
Mwaka 2015 kesi yake ikaanza kusikilizwa, na mwaka 2019 akapatikana na hatia katika makosa 18, yakiwemo ubakaji, mauaji ya raia wasio na hatia, na kutumikisha watoto jeshini. Akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, adhabu ambayo anaitumikia hadi sasa.